Showing posts with label bongo actors. Show all posts
Showing posts with label bongo actors. Show all posts

Saturday, March 08, 2014

RAY‘MGONJWA WA HIP HOP

VINCENT Kigosi ‘ Ray ’ amedhihirisha kuwa
anapenda sana kusikiliza muziki wa Hip Hop
kuliko muziki mwingine.
Hivi karibuni, baada ya Ray kukiri kuwa
anaupenda muziki huo, paparazi wetu
alikaa naye kwa zaidi ya saa tano ambapo
muda wote alisikiliza muziki huo hususan
wimbo wa Gere wa Kundi la Weusi

Thursday, March 06, 2014

SETH:KANUMBA ANANITOKEA

SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu
Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu
za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo
ya kushangaza , akidai kaka yake huyo
amekuwa akimtokea ndotoni.
Marehemu Steven Kanumba.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa
Kampuni ya Kanumba The Great Film baada
ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili
07, 2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican ,
jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari hizi ,
wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam , kwa
sauti ya huzuni, Seth alisema : “ Kiukweli sina
amani, hii hali inanitesa sana . Kila mara
ananitokea ndotoni na kunieleza mambo
yanayofanana. ”
MAMBO GANI ?
“ Analalamika kwa nini eti ofisi yake
aliyoiacha haina mafanikio . Sasa nashindwa
kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia .
Analalamika kwa nini filamu hazitolewi , ni
jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo
wangu, ” alisema Seth.
Seth Bosco.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH : Nikiwa usingizini , nakuwa kama
naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya
moja kwa moja .. . ndoto ikikatika , nashtuka
na kujikuta nahema kwa kasi.
AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“ Mara ya tatu sasa, ndiyo maana
nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza
ni kwamba , kila anaponitokea , lazima
nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa
kasi na kutoka jasho jingi .
“ Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini
alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona
hili suala siyo la kulikalia kimya , ikabidi
nimwambie mama . ”
MAMA KANUMBA ANASEMAJE ?
“ Mama alishtuka na ameshangazwa sana na
hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara
ngapi , nikamwambia tatu , akasema lazima
tufanye maombi kuondoa hali hiyo , ” alisema
Seth huku akionesha uso wa wasiwasi

Soma alichoandika mcheza filamu Bond Bin Sinnan siku ya birthday ya Farheen kwenye ukurasa wake wa facebook

Happy birthday Farheen Juma Kilowoko mungu
akupe afya, umri, akili timamu za kuijua dunia na
yeye Allah pia bila kusahau ukujaalie Upendo kwa
watu wote wao wakupende nawe uwapende
amiiiiin....thank u Wastara kwa
mualiko .....haahhaahaha chitaki pichaaaa..

Wednesday, March 05, 2014

Tuesday, February 25, 2014

DK.CHENI:FREEMASON WANANITESA

MINONG’ ONO na uvumi unaotambaa kwa
kasi kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi
huru (Freemasons ), unazidi kumtesa msanii
wa filamu za Kibongo , Mahsein Awadhi Said
‘Dk . Cheni ’ kwa madai ya kwamba anajisikia
vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya
wadau wa tasnia hiyo .
Dk . Cheni .
Mwishoni mwa wiki iliyopita , mwandishi
wetu alisikia fununu kutoka kwa wadau
wengi wa filamu wakiwemo wasanii
wenzake wakidai kuwa Dk . Cheni ni
mwanachama halali wa taasisi hiyo ndiyo
maana mambo yake ni mazuri kifedha
ukilinganisha na wasanii wengine
wanaoaminika kuwa na uwezo mkubwa wa
kuigiza kuliko yeye .
“ Kila dalili inaonesha kabisa Dk . Cheni ni
Freemason , angalia mavazi yake mengi ni
meusi , machata na alama kibao
zinazohusishwa na taasisi hiyo, angali fedha
aliyonayo, angalia hata gari lake lilivyojaa
alama za ajabu ajabu, huyu jamaa ni
Freemason kabisa , ” alisema mdau mmoja
wa filamu ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini alipozungumza na
mwandishi wetu .
Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa
nyakati tofauti na baadhi ya wasanii
wenzake .
Dk . Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu
Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai
hayo alikuwa na haya ya kusema :
“ Dah! na wewe umeyapata kaka ? Hakika
naumia sana na madai hayo , yamevuma
sana kwa wadau , tena baadhi yao ni watu
ninaowaheshimu sana, jamani mimi siyo
Freemason , naigiza , kazi zangu za u - MC
zinaniingizia kipato, najiwekea akiba .
“ Si mtu wa starehe , nawekeza katika
biashara ndogondogo, madai haya ya
Freemason yananitesa sana ila namwachia
Mungu , ” alisema Dk . Cheni .

Saturday, February 22, 2014

MASTAA WAKOMALIA BUNGE LA KATIBA

BAADHI ya mastaa wa Bongo Movies
wameamua kujitoa kinaga ubaga kwenda
Dodoma kwa ajili ya kuweka msisitizo kwa
wabunge wa Bunge la Katiba juu ya maslahi
ya kazi zao .

Taarifa zinaeleza kuwa, miongoni mwa
mastaa ambao wamekita kambi pande za
Dodoma ni pamoja na Rais wa Shirikisho la
Sanaa Nchini , Siamon Mwakifwamba pamoja
na Kulwa kikumba ambaye
amefafanua uwepo wao mjini humo :
“ Tunataka kuhakikisha bunge hili la katiba
linatuthamini katika suala zima la kutetea
maslahi ya kazi zetu , huu ni muda wa
wasanii kuamka, tuzalishe fedha kulingana
na jasho letu , ” alisema Dude.

Monday, February 17, 2014

Huyu ndio Philimon Lutwaza au uncle D

Mcheza filamu za kibongo anaejizolea umaarufu siku hadi siku kutokana na kufanya vizuri kwenye filamu ya ‘After death‘ Philimon Lutwaza au Uncle D ameaidi kufanya makubwa mwaka huu

Akimwagia data muandishi wa habari hii amesema mwaka huu amejipanga vizuri na anajua utakuwa wa neema sana kwake kwakua anaamini anakipaji na yupo kwenye sanaa muda mrefu

‘Kwenye filamu ya ‘after death ya Wolper mimi nimecheza kama Uncle D yani baada ya Uncle JJ kufa mi ndio naishi na wale watoto Jenipher na Patrick

Saturday, February 15, 2014

Bond Bin Sinnan na Linex Sunday ndio mastaa wa bongo waliozaliwa siku ya Valentine

Msanii wa bongo fleva Linex Sunday na mcheza filamu za kitanzania ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha runinga ‘Action&cut‘Bond bin Sinnan ndio mastaa wa Tanzania waliozaliwa siku ya Valentine.

Kupitia ukurasa wake wa facebook Bond ameandika ujumbee huu kumshukuru mwenyezi mungu soma hapo chini

Asante mola ulietukuka hakika Siena cha
kukulipa kwa wema wako kwangu... Ni mengi
uliyonitendea alhamdulillah kwa kunijaalia umri
huu na baraka.. happy birthday kwangu
tena ....niongoze na uzidi Kunijaalia furaha, afya
na mafanikio huko niendako hakika we ndo kila
kitu kwangu.... pia siwezi wasahau wazazi, ndugu
zangu na marafiki zangu nashukuru kwa kuwa na
Mimi Kipindi chote....happy birthday Bond Bin
Sinnan

Stanley Msungu:waacheni watu wa comedy wafanye kazi yao

Sio kwa ugomvi ila kama kunamtu ntamkwaza
anisamehe ni mawazo na nijinsi ya kuonyesha
upendo kwenu, hivi nyinyi mnaojihisi mnauza
sana kwenye kiwanda chetu cha muv mnajua
kama mnafanya comed mkihisi watanzania
wanafrahia kumbe mnatupa shida wanaharakati
waacheni watu wa comed wafanye kazi yao, sina
maana kuwashirikisha watu wa comed ni tatizo
tatizo ni sisi tunawashirikisha alafu na sisi
tunafanya comed ok sio mbaya mtu akiamua
kufanya comed sasa mbona ubunifu kama
umewaishia hivi kila muv lazima ulazimishe
majuto awepo? Ok hayanihusu ngoja tuone
bongo muv inavyokwenda ila mm nashauli
tuendelee kuandaa mashamba tayal kwa kulima,
one luv.

Facebook

Tuesday, February 11, 2014

Kumbe Bond Bin Sinnan amezaliwa valentine day?

Muogozaji wa filamu mwenye uwezo mkubwa bongo na mtangazaji maarufu wa kipindi cha television cha action&cut Bond Bin Sinnan ameanza kupokea zawadi za sherehe ya siku yake ya kuzaliwa kupitia akaunti yake ya facebook ameandika hivi

“Bond Bin Sinnan
Soon 2 b born...zawadi jamani naanza kupokea
Leo maana tar 14 mtakuwa bizy na wachuchu na
Mimi ndo birthday yanguu.......“

Bond bin sinnan

MAISHA YA MSANII MASANJA MAKANDAMIZAJI NDIO HAYA

Masanja Mkandamizaji si geni masikioni mwao
kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu
watazamaji pale anapoonekana katika runinga
na Kundi la Original Comedy.
Licha ya kufika hapo alipo sasa, msanii huyu
anakiri wazi kuwa amepitia katika ugumu
hususani wakati alipoamua kuanza maisha
binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka
nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake
alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na
kuanza maisha binafsi kama kijana .
Nilimwambia dada anitafutie chumba na
alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama
nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya
Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya
Sh5000 kwa mwezi, anasema Masanja.
Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha
ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa
kwani licha ya kuwa katika hali ngumu
hakukata tama bali alizidi kujituma kwa nguvu
zake zote.
Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata
hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa
inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda
unapofikia wakati kulipa kodi.
Yaani hiyo Sh5000 kuipata ilikuwa shughuli
maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa
mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama
mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema.
Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku
alipofanikiwa kupata fedha kidogo
iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo
ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua
kwa jasho lake.
Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau
marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu
mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na
mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo
sasa .
Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa
anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda
kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa
kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha
yalikuwa magumu.
Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata
ya kununua chipsi kavu lakini siku moja
nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki
moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya
kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa
nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia
kumenya viazi kwa washikaji,
Sambamba na uchekeshaji Masanja pia
amejiingiza katika shughuli za kumtukuza
Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya
vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na
kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili
ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini
ya jua.

John Minja

Sunday, February 09, 2014

BODI YA FILAM TANZANIA IMEPITILIZA KUHUSU SUALA LA MAADILI

Bishop Hiluka aliwahi kuandika kuwa tunahitaji
BODI HURU YA FILAMU nchini tofauti na iliyopo
sasa ambayo haipo huru na kama haijui kazi
inayoifanya. Mimi nakubaliana kabisa na Hiluka
kwa kuwa bodi hii haielweki kwa kuwa mara
nyingi inalalamikiwa na wasanii kwa kuzuia kazi
zao bila sababu za msingi kwa madai ya kulinda
maadili ilihali kinachozungumziwa katika filamu
husika ni kitu ambacho kipo katika jamii zetu
na wakati mwingine hata filamu haihitaji
kuzuiliwa but inazuiliwa kama ilivyotokea kwa
filamu ya Dr. Cheni "Nimekubali Kuolewa" kwa
madai eti juu ya kava kavaa vazi la shera na
kujipodoa sana !. kwa mujibu wa Dr.Cheni
filamu hii inaonyesha madhara ya mapenzi ya
jinsia moja(ushoga). Vipi kuhusu kina Joti katika
Ze Comedy mbona bodi haiwapigi marufuku !.
Ikumbukwe kuwa wakati ugonjwa wa UKIMWI
ulipoingia duniani serilali ya Tanzania ilikuwa
inasita kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo
mashuleni kwa madai ya kulinda maadili lakini
vijana wengi walipoanza kupukutika kwa
ugonjwa huo kwa kukosa elimu ya kujikinga
ndipo serikali ikaamka na kuanza kutoa elimu
mashuleni kuhusu ugonjwa huo.
Tuseme bodi ya filamu Tz haioni filamu za
vitendo vya ngono kutoka nje ya nchi why
zisipigwe marufuku kuingia nchini badala yake
zimejaa sokoni huku bodi ikizuia kukua kwa
tasnia ya filamu kwa kigezo cha maadili ! ni
kweli maadili ni kitu muhimu lakini wengi
wanakubali bodi ya filamu Tz imepitiliza kwa
hayo maadili. Kwasasa ni vigumu wasanii
kuigiza filamu inayoonyesha uozo wa viongozi
wa juu nchini kwani bodi itazuia filamu kwa
kigezo cha maadili. Kingine katika hivi vyombo/
taasisi za kukuza tasnia ya filamu nchini
wengine wamepewa uongozi wa kuongoza
taasis husika ilihali hawajui nini maana ya
filamu na sanaa kwa ujumla.
Mfano katika filamu ya Nairobi Half Life(2012)
kutoka nchini Kenya kulikuwa na tukio la
mmoja wa wahusika wakuu(vijana wa kiume)
kunyosheana kidole cha kati kinachoashiria
matusi ili kuleta uhalisia wa baadhi ya lugha za
ishara zinazotumiwa na vijana hasa wa mtaani,
filamu hii ni moja ya filamu chache nzuri
zilizotengenezwa kwa lugha ya Kiswahili kiasi
cha kupenya kwenye hatua ya awali katika tuzo
za Oscars. Lakini kama hii filamu
ingetengenezwa Tanzania ni lazima ingezuiliwa
na Bodi ya filamu kwa tukio hilo la
kunyosheana kidole cha kati kwa madai sio
maadili na matokeo yake uhalisia kuondoka
kama filamu zetu nyingi zilivyo. kama ni hivyo
sasa hayo madaraja ya filamu huwa
yanawekwa kwa ajili gani ! si waweke daraja
moja tu linaloitwa "MAADILI" ili kila mtu ajue!
Kuna Professor mmoja wa chuo kikuu nchini
aliwahi kuwa mmoja wa viongozi pale BASATA
siku moja nilimuuliza kwanini chuo
unachofundisha wasanii wa filamu nchini
wanasema hawaruhusiwi kurekodi hapa ilihali
wewe ni mmoja wa viongozi wa idara ya sanaa
chuoni hapa jibu lake lilikuwa "serikali
haieleweki" hii ina maana kuwa hawa viongozi
wakati mwingine wanakuta mfumo mbovu wa
taasisi lakini wanashindwa kuubadilisha ni
kama ilivyo hapo bodi ya filamu sasa kila kitu
itakuwa ni kulinda maadili. Bikini kuvaliwa
kwenye filamu ya kitanzania ni issue lakini
katika video za muziki wa Bongofleva kuvaa
bikini hakuna tatizo kabisa, hivi katika maadili
kuna Tanzania 2! -yaani Tanzania ya filamu
(yenye maadili) na Tanzania ya Bongofleva(isiyo
na maadili kwa kuvaa bikini katika music
videos), lakini mbona bikini ni vazi la ufukweni
na hata kwa khanga au kitenge vyenye asili ya
Afrika/tanzania vyaweza kutumika kushonea
vazi hilo kwa msanii akiwa na scenes za beach !
Wasanii kibao wanalalamikia bodi kwa kuwa na
longolongo katika makava ya filamu kuwa
hayana maadili hata kama ni mpasuo tu wa
gauni la msanii wa kike anatakiwa akapige
picha ya kava upya.
Kwa ufupi ni kuwa mapenzi ya jinsi moja
hayakubaliki katika jamii nyingi duniani kote,
hata katika filamu za Bollywood suala hili
halipewi uzito mkubwa kwa kigezo hicho cho
cha maadili , filamu za Bollywood huonyesha
suala la mapenzi ya jinsia moja ki-comedy zaidi
kuliko katika filamu serious lakini wasanii mara
nyingi huitwa na bodi na kukaa vizuri kufanya
majadiliano ya pamoja ili kuweka kazi vizuri
katika kupokelewa na jamii hasa katika
kufikisha ujumbe. Tofauti na Hollywood ambapo
filamu huwa jambo la kawaida kuonyesha
mapenzi ya jinsia moja kwa kuwa jamii zao
nyingine zimebariki kabisa suala hilo. Hivyo
bodi ya filamu Tanzania ijitazame upya kwani
imekuwa ikilalamikiwa sana kuwa inabana sana
kazi za wasanii hata pale pasipo na tatizo
kubwa badala ya kukuza tasnia ya filamu nchini
bodi imekuwa ni moja ya vyombo
vinavyolalamikiwa kuifanya tasnia ya filamu
nchini isusuesue.

source: Swahiliworldplanet

Thursday, February 06, 2014

DUDE NAYE ALILIA UBUNGE

WIMBI la wasanii kuingia kwenye siasa
limeendelea kushika kasi ambapo awamu hii
msanii wa maigizo na filamu Bongo, Kulwa
Kikumba ‘ Dude’ ametangaza kugombea
ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa
mwaka 2015.

‘Akistorisha ’ na paparazi wetu , Dude alisema
kutokana na sanaa kutotoa masilahi
ipasavyo , ameamua kuingia kwenye ulingo
wa siasa ambapo anatarajia ‘ kunyakua’
Jimbo la Tabora Mjini ambalo kwa sasa
linaongozwa na Mwenyekiti wa Klabu ya
Simba, Ismail Aden Rage .
“ Natarajia kugombea ubunge nyumbani
kwetu Tabora mjini , niko tayari kuchuana na
Rage na kwa sasa nipo katika maandalizi
ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani
wananikubali sana, hivyo natarajia ushindi
tu, ”

GP

Thursday, January 30, 2014

UKATA WAKWAMISHA KAZI ZA DUDE

HALI ya uchumi ya mwigizaji Kulwa Kikumba
‘Dude’ imemkwamisha mwigizaji huyo
ashindwe kurekodi tamthiliya yake .

Akizungumza na paparazi wetu , Dude alikiri
kuwa uchumi umemkalia vibaya ambapo
aliruhusiwa kupewa muda wa hewani katika
Runinga ya East Africa lakini akashindwa
kushuti kutokana na majukumu ya kifamilia
kumuandama .
“ Daa we acha tu , mwezi wa kwanza huu
majanga matupu. Nimeshindwa , kama
unavyojua nina watoto wengi mambo ya
ada yamenibana kwelikweli , ” alisema Dude
ambaye ana jumla ya watoto sita kwa
mama tofauti

GP

Tuesday, January 28, 2014

MZEE DUDE WA FUTUHI HATUNAYE TENA

MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na
uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia
akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo
jijini Mwanza leo jioni!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema
peponi. AMEN!

SHIJA ATONGOZWA NA SHOGA

MSANII wa filamu za Kibongo, Deogratius
Shija hivi karibuni alijikuta katika wakati
mgumu baada ya kutongozwa na shoga .
Deogratius Shija .
Akitema mbili tatu na paparazi wetu , Shija
alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni
katika Ukumbi wa Traventine - Magomeni ,
Dar ambapo alitoka na kwenda msalani
akiwa hajui hili wala lile alishtuka baada ya
kumsikia mwanaume akimpapasa huku
akimwambia kuwa anampenda .
“ Nilimshtukia kumbe ni shoga . Mapenzi ya
jinsia moja ni dhambi kubwa sana kwa
Mungu , sijawahi na sitaweza kufanya
dhambi hiyo milele mimi ni Mkristo
niliyekamilika, nawashangaa wanaume
wanaofanya uchafu huo , ” alisema Shija.

GP

Monday, January 27, 2014

STEVE:KAMA SI USANII NINGEKUWA MAHAKAMANI

MCHEKESHAJI maarufu Bongo.   Steven Mengere ‘ Steve Nyerere’ amesema kama
asingekuwa msanii basi angekuwa
mfanyakazi wa mahakama.

Akistorisha na paparazi wetu juzikati, Steve
Nyerere alisema kuwa kila msanii anatakiwa
kujiuliza kama siyo kazi ya usanii angekuwa
anafanya kazi gani lakini kwa upande wake
yeye angekuwa mfanyakazi wa mahakama
kwani anaipenda kazi hiyo.
“ Huwa najiuliza mara kwa mara lakini siku
zote naamini isingekuwa sanaa ningekuwa
mfanyakazi wa mahakamani , napenda
kuwapeleka watu lupango, kazi nzuri sana , ”
alisema Steve Nyerere .

GP

MSANII KAOLE AVUNJIKA MGONGO

MSANII wa Kundi la Kaole Sanaa , Zaina
Ramadhan ‘ Nandi’ anasumbuliwa na
ugonjwa wa mifupa akidai kuvunjika pingili
za mgongo kisha kushindwa kutembea na
kufanya kazi zake za sanaa na nyinginezo.
Zaina Ramadhan ‘ Nandi’ .
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi
karibuni, Nandi alisema kuwa alianza
kuumwa baada ya kupata hitilafu mwaka
2012 alipokuwa akitoka Chuo cha Sanaa
pale Lego , Ubungo jijini Dar.
Nandi alisema siku ya tukio alikuwa akivuka
barabara ambapo alishangaa kuona mguu
umesita ghafla akashindwa kutembea hadi
watu wakambeba kumsaidia kuvuka.
“ Sikujua kilichonipata, nikaenda nyumbani
wakanichua na mafuta ya asili ambayo
yalinisaidia kidogo lakini tatizo lilizidi kuwa
kubwa. Nikiwa nyumbani mama aliniomba
nimsaidie kubeba vyombo lakini nilishindwa
kuinua beseni baada ya kuinama na pingili
za mgongo zikavunjika , ” alisema Nandi.
Baada ya hapo , Nandi alisema alikwenda
Hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni jijini
Dar ambapo alimuona daktari akamuandikia
dawa za kutuliza maumivu na kumhamishia
Muhimbili kwa uchunguzi zaidi .
“ Hapa nilipo sina uwezo kabisa kwani dawa
nilizoandikiwa zinauzwa ghali sana, familia
imejitahidi kunisaidia lakini bado,
nawaomba Watanzania wanisaidie ili nipate
matibabu kwani sielewi tatizo langu ni nini
kutokana na kukosa vipimo , ” alisema Nandi.
Nandi amewahi kucheza filamu mbalimbali
ikiwemo Yatima , Jua la Kiama , Kuzaa si
Kupata na nyingine nyingi.
Kwa aliyeguswa na tatizo la msanii huyo na
mwenye nia ya kumsaidia , awasiliane naye
kwa namba 0684501177

GP

Thursday, January 16, 2014

MZEE CHILO AWATOLEA UVIVU WASANII

MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Ahmed Ollotu ‘Mzee Chilo’ amewatolea uvivu wasanii wasiopenda kushirikiana na wenzao katika matatizo na kuwaonya kuwa tabia hiyo si nzuri kwani ipo siku itawaponza.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika mahojiano maalumu, Chilo aliyejizolea heshima na umaarufu mkubwa katika fani hiyo, alikiri kuwa wasanii wengi wamekuwa wakijitenga na wenzao wakati wa matatizo jambo ambalo linakera na kuumiza.

Msanii huyo alisema hakuna binadamu anayejua hatima ya maisha yake hapa duniani, hivyo ni vyema kuishi katika mwenendo ulio mzuri, kwani watu wote ni udongo na mavumbini watarejea.

GP

Monday, January 06, 2014

Filamu ya Last Decision ni nzuri sana:Bondi Bin Sinnan

Muongozaji wa filamu mwenye jina kubwa Tanzania Bond Bin Sinnan amesema filamu mpya ya Wastara Sajuki “Last Decision“ni nzuri sana kwa kua ina stori,location nzuri na wahusika wamecheza kwa kiwango cha juu

“Ni movie nzuri watu wamecheza vizuri na story ni nzuri pia locations Ni nzuri“

Filamu hiyo ameiongoza Bond mwenyewe na kuongeza kuwa kuna baadhi ya vipande vilimpa ugumu kuongoza kama kile cha Wastara kuwa kichaa na baadhi ya vipande vya wasanii chipukizi

Last Decision imechezewa mkoani Mwanza na imewashirikisha Wastara na Hemedy na wasanii wenginge wengi inatoka hivi karibuni