Friday, January 17, 2014

Jackline Wolper ameamza kumuweka bayana mchumba wake wa sasa

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.

Akizungumza hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo.

“Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.

Wolper aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja  kwa wazazi wa pande zote mbili ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.

GP

No comments:

Post a Comment