SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu
Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu
za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo
ya kushangaza , akidai kaka yake huyo
amekuwa akimtokea ndotoni.
Marehemu Steven Kanumba.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa
Kampuni ya Kanumba The Great Film baada
ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili
07, 2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican ,
jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari hizi ,
wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam , kwa
sauti ya huzuni, Seth alisema : “ Kiukweli sina
amani, hii hali inanitesa sana . Kila mara
ananitokea ndotoni na kunieleza mambo
yanayofanana. ”
MAMBO GANI ?
“ Analalamika kwa nini eti ofisi yake
aliyoiacha haina mafanikio . Sasa nashindwa
kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia .
Analalamika kwa nini filamu hazitolewi , ni
jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo
wangu, ” alisema Seth.
Seth Bosco.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH : Nikiwa usingizini , nakuwa kama
naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya
moja kwa moja .. . ndoto ikikatika , nashtuka
na kujikuta nahema kwa kasi.
AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“ Mara ya tatu sasa, ndiyo maana
nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza
ni kwamba , kila anaponitokea , lazima
nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa
kasi na kutoka jasho jingi .
“ Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini
alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona
hili suala siyo la kulikalia kimya , ikabidi
nimwambie mama . ”
MAMA KANUMBA ANASEMAJE ?
“ Mama alishtuka na ameshangazwa sana na
hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara
ngapi , nikamwambia tatu , akasema lazima
tufanye maombi kuondoa hali hiyo , ” alisema
Seth huku akionesha uso wa wasiwasi
Thursday, March 06, 2014
SETH:KANUMBA ANANITOKEA
Labels:
bongo actors
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment