Tuesday, February 25, 2014

DK.CHENI:FREEMASON WANANITESA

MINONG’ ONO na uvumi unaotambaa kwa
kasi kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi
huru (Freemasons ), unazidi kumtesa msanii
wa filamu za Kibongo , Mahsein Awadhi Said
‘Dk . Cheni ’ kwa madai ya kwamba anajisikia
vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya
wadau wa tasnia hiyo .
Dk . Cheni .
Mwishoni mwa wiki iliyopita , mwandishi
wetu alisikia fununu kutoka kwa wadau
wengi wa filamu wakiwemo wasanii
wenzake wakidai kuwa Dk . Cheni ni
mwanachama halali wa taasisi hiyo ndiyo
maana mambo yake ni mazuri kifedha
ukilinganisha na wasanii wengine
wanaoaminika kuwa na uwezo mkubwa wa
kuigiza kuliko yeye .
“ Kila dalili inaonesha kabisa Dk . Cheni ni
Freemason , angalia mavazi yake mengi ni
meusi , machata na alama kibao
zinazohusishwa na taasisi hiyo, angali fedha
aliyonayo, angalia hata gari lake lilivyojaa
alama za ajabu ajabu, huyu jamaa ni
Freemason kabisa , ” alisema mdau mmoja
wa filamu ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini alipozungumza na
mwandishi wetu .
Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa
nyakati tofauti na baadhi ya wasanii
wenzake .
Dk . Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu
Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai
hayo alikuwa na haya ya kusema :
“ Dah! na wewe umeyapata kaka ? Hakika
naumia sana na madai hayo , yamevuma
sana kwa wadau , tena baadhi yao ni watu
ninaowaheshimu sana, jamani mimi siyo
Freemason , naigiza , kazi zangu za u - MC
zinaniingizia kipato, najiwekea akiba .
“ Si mtu wa starehe , nawekeza katika
biashara ndogondogo, madai haya ya
Freemason yananitesa sana ila namwachia
Mungu , ” alisema Dk . Cheni .

No comments:

Post a Comment