Masanja Mkandamizaji si geni masikioni mwao
kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu
watazamaji pale anapoonekana katika runinga
na Kundi la Original Comedy.
Licha ya kufika hapo alipo sasa, msanii huyu
anakiri wazi kuwa amepitia katika ugumu
hususani wakati alipoamua kuanza maisha
binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka
nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake
alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na
kuanza maisha binafsi kama kijana .
Nilimwambia dada anitafutie chumba na
alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama
nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya
Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya
Sh5000 kwa mwezi, anasema Masanja.
Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha
ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa
kwani licha ya kuwa katika hali ngumu
hakukata tama bali alizidi kujituma kwa nguvu
zake zote.
Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata
hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa
inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda
unapofikia wakati kulipa kodi.
Yaani hiyo Sh5000 kuipata ilikuwa shughuli
maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa
mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama
mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema.
Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku
alipofanikiwa kupata fedha kidogo
iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo
ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua
kwa jasho lake.
Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau
marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu
mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na
mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo
sasa .
Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa
anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda
kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa
kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha
yalikuwa magumu.
Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata
ya kununua chipsi kavu lakini siku moja
nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki
moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya
kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa
nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia
kumenya viazi kwa washikaji,
Sambamba na uchekeshaji Masanja pia
amejiingiza katika shughuli za kumtukuza
Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya
vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na
kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili
ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini
ya jua.
John Minja
No comments:
Post a Comment