Msanii wa kike katika filamu za kibongo Wastara Sajuki amesema kwenye filamu yake mpya ya Shaymaa amemuweka Salma Nisha kwa kua ni muigizaji mwenye uwezo mkubwa na anajua anachokifanya
Amesema sababu nyingine stori ilikua inataka mtu anaefanana nae kawa rangi na kimwili hivyo akaona Nisha ndio chaguo sahihi
Kwa upande wake Niasha amesema amefurai kucheza filamu hiyo kwani alikua anampenda Wastara tangu akiwa kidato cha pili hivyo ametimiza ndoto yake ya muda mrefu
Aidha amesema kwenye filamu hiyo amecheza kama Shaymaa na kuwaomba mashabiki wainunue kwa wingi itakapotoka ili waone alichokifanya
Filamu ya Shaymaa inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu na wamo Yusuph Mlela,Salma Nisha na waigizaji wengine wengi
No comments:
Post a Comment