BAADHI ya mastaa wa Bongo Movies
wameamua kujitoa kinaga ubaga kwenda
Dodoma kwa ajili ya kuweka msisitizo kwa
wabunge wa Bunge la Katiba juu ya maslahi
ya kazi zao .
Taarifa zinaeleza kuwa, miongoni mwa
mastaa ambao wamekita kambi pande za
Dodoma ni pamoja na Rais wa Shirikisho la
Sanaa Nchini , Siamon Mwakifwamba pamoja
na Kulwa kikumba ambaye
amefafanua uwepo wao mjini humo :
“ Tunataka kuhakikisha bunge hili la katiba
linatuthamini katika suala zima la kutetea
maslahi ya kazi zetu , huu ni muda wa
wasanii kuamka, tuzalishe fedha kulingana
na jasho letu , ” alisema Dude.
No comments:
Post a Comment