Monday, January 27, 2014

MSANII KAOLE AVUNJIKA MGONGO

MSANII wa Kundi la Kaole Sanaa , Zaina
Ramadhan ‘ Nandi’ anasumbuliwa na
ugonjwa wa mifupa akidai kuvunjika pingili
za mgongo kisha kushindwa kutembea na
kufanya kazi zake za sanaa na nyinginezo.
Zaina Ramadhan ‘ Nandi’ .
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi
karibuni, Nandi alisema kuwa alianza
kuumwa baada ya kupata hitilafu mwaka
2012 alipokuwa akitoka Chuo cha Sanaa
pale Lego , Ubungo jijini Dar.
Nandi alisema siku ya tukio alikuwa akivuka
barabara ambapo alishangaa kuona mguu
umesita ghafla akashindwa kutembea hadi
watu wakambeba kumsaidia kuvuka.
“ Sikujua kilichonipata, nikaenda nyumbani
wakanichua na mafuta ya asili ambayo
yalinisaidia kidogo lakini tatizo lilizidi kuwa
kubwa. Nikiwa nyumbani mama aliniomba
nimsaidie kubeba vyombo lakini nilishindwa
kuinua beseni baada ya kuinama na pingili
za mgongo zikavunjika , ” alisema Nandi.
Baada ya hapo , Nandi alisema alikwenda
Hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni jijini
Dar ambapo alimuona daktari akamuandikia
dawa za kutuliza maumivu na kumhamishia
Muhimbili kwa uchunguzi zaidi .
“ Hapa nilipo sina uwezo kabisa kwani dawa
nilizoandikiwa zinauzwa ghali sana, familia
imejitahidi kunisaidia lakini bado,
nawaomba Watanzania wanisaidie ili nipate
matibabu kwani sielewi tatizo langu ni nini
kutokana na kukosa vipimo , ” alisema Nandi.
Nandi amewahi kucheza filamu mbalimbali
ikiwemo Yatima , Jua la Kiama , Kuzaa si
Kupata na nyingine nyingi.
Kwa aliyeguswa na tatizo la msanii huyo na
mwenye nia ya kumsaidia , awasiliane naye
kwa namba 0684501177

GP

No comments:

Post a Comment