Thursday, February 06, 2014

DUDE NAYE ALILIA UBUNGE

WIMBI la wasanii kuingia kwenye siasa
limeendelea kushika kasi ambapo awamu hii
msanii wa maigizo na filamu Bongo, Kulwa
Kikumba ‘ Dude’ ametangaza kugombea
ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa
mwaka 2015.

‘Akistorisha ’ na paparazi wetu , Dude alisema
kutokana na sanaa kutotoa masilahi
ipasavyo , ameamua kuingia kwenye ulingo
wa siasa ambapo anatarajia ‘ kunyakua’
Jimbo la Tabora Mjini ambalo kwa sasa
linaongozwa na Mwenyekiti wa Klabu ya
Simba, Ismail Aden Rage .
“ Natarajia kugombea ubunge nyumbani
kwetu Tabora mjini , niko tayari kuchuana na
Rage na kwa sasa nipo katika maandalizi
ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani
wananikubali sana, hivyo natarajia ushindi
tu, ”

GP

No comments:

Post a Comment