Thursday, January 16, 2014

DEVOTHA MBAGA ANASA

MSANII aliyefanya poa kwenye filamu kadhaa ikiweko ya Malaika, Devotha Julius Mbaga ‘The First Born’ yuko katika wakati mgumu kufuatia kunasa ujauzito ambao kwa sasa siyo siri tena.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, mmoja wa rafiki wa msanii huyo (jina kapuni) alisema kuwa licha ya msanii huyo kufanya siri juu ya ujauzito huo, lakini kwa sasa dalili zinaonesha kuwepo kwa ujauzito na kwamba kwa sasa anatumia muda mwingi kuwa nyumbani ili kukwepa macho ya wengi kugundua juu ya kubugia kwake ‘kijusi’.

“Kwa sasa Devotha ana mimba, lakini anafanya siri kubwa sana ili watu wengi wasijue (wakiwemo waandishi), ndiyo maana haonekani mara kwa mara, anatumia muda mwingi kuwa nyumbani,” kilisema chanzo hicho.

Devotha alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, amekiri kuwa na kitumbo cha miezi minne.

No comments:

Post a Comment