Thursday, January 16, 2014

MZEE CHILO AWATOLEA UVIVU WASANII

MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Ahmed Ollotu ‘Mzee Chilo’ amewatolea uvivu wasanii wasiopenda kushirikiana na wenzao katika matatizo na kuwaonya kuwa tabia hiyo si nzuri kwani ipo siku itawaponza.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika mahojiano maalumu, Chilo aliyejizolea heshima na umaarufu mkubwa katika fani hiyo, alikiri kuwa wasanii wengi wamekuwa wakijitenga na wenzao wakati wa matatizo jambo ambalo linakera na kuumiza.

Msanii huyo alisema hakuna binadamu anayejua hatima ya maisha yake hapa duniani, hivyo ni vyema kuishi katika mwenendo ulio mzuri, kwani watu wote ni udongo na mavumbini watarejea.

GP

No comments:

Post a Comment