Thursday, March 23, 2017

CASSIE KABWITA KUJA NA "KWACHA"

 Mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Zambia Cassie Kabwita amesema filamu yake ya 'KWACHA"inamafunzo makubwa kwenye familia za kiafrika.
Amesema filamu hiyo inafundisha jinsi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia,unyanyasaji wa kijinsia,wivu pamoja na kufundisha  upendo wa kweli
Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema kwenye filamu hiyo amewashirikisha mastaa wenye majina makubwa nchini Tanzania Vicent Kigosi (ray) na Kajala Masanja uku yeye na waigizaji wengine kutoka nchini Zambia akiwemo Owas Mwape wakifanya makubwa kwenye filamu hiyo

RACHEL YUPO HONEYMOON MOROGOROOO!

 MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Swahilihood Rachel Bitulo yupo mkoani Morogoro kikazi akirekodi filamu inayokwenda kwa jina la Honeymoon huku yeye akiwa kinara wa sinema hiyo akishirikiana na staa kibao wa Mkoani humu amesema Rachel Bitulo staa wa filamu ya Nimekosea wapi?
 “Kwa sasa nipo busy sana kwani narekodi filamu ya huku Morogoro ni kazi nzuri sana najua itazidi kuniweka pazuri zaidi katika tasnia ya filamu Bongo sinema yenyewe inaitwa Honeymoon,”.
Rachel amesema kuwa filamu hiyo imetayarishwa na mtayarishaji wa Mkoani Morogoro anaitwa Bravo ambaye amejitambulisha kwa jina moja tu, pia katika filamu hiyo yupo mwwigizaji mwingine anayejulikana kwa jina la Idrisa Makupa aka Kupa sambamba na wasanii nyota kutoka Moro.

WASTARA AMETUSOGEZEA VIDEO HII HAPA YA WIMBO WAKE WA HAPENDEKI

WASTARA JUMA ANARUDI UPYA NA "HAPENDEKI"

LUTWAZA KUZIBA PENGO LA KANUMBA KWENYE FILAMU

 Mcheza filamu anaefanya vizuri kwenye tasnia Philemon Lutwaza ametajwa kuwa ndio mwenye jukumu la kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba kutokana na kufanana kwa muonekano na uigizaji wake

Wakifunguka kiafrika bila hofu yoyote baadhi ya mashabiki wamesema Lutwaza anaweza kuziba pengo kwani anajituma sana kwenye kazi na hajatofautiana sana na marehemu Kanumba

"Unajua huyu Lutwaza anacheza vizuri sana na nina vutiwa na uigizaji wake anajua yani nikimuangalia namuona Kanumba kabisa"

Lutwaza anaonekana kwenye filamu ya Yai viza ambayo imeandaliwa na muongozaji wa filamu nchini Sulesh Mala

CLOUD 112 AWAVUTA WASTARA NA BARAFU SWEDEN KUFANYA MOVIE YA USIJISAHAU


  Wasanii wenye majina makubwa bongo movie Wastara Juma na Suleiman Barafu wapo nchini Sweden wakifanya stage play kwa watanzania wanaoishi nchini humo,kwa lengo la kuwaelimisha mambo mbalimbali ya kimaisha kupitia sanaa za jukwaani


 Aidha Wastara na Barafu wako nchini humo pia kwa maandalizi ya filamu ya Usijisahau inayoandaliwa na mcheza filamu mkongwe nchini Cloud 112
  Filamu hiyo yenye maudhui ya kislamu inaenga kuwafumbua macho watu,waishi kwa kumtegemea mungu wasijisahu wafanye ibada




Saturday, December 03, 2016

UZINDUZI WA SIRI YA MOYO WAFANYIKA DAR ES SALAAM











Uzinduzi wa filamu ya Siri ya moyo umefanyika kwenye ukumbi wa sinema Suncrest ulipo ndani ya jumba la biashara,Quality centre na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa filamu nchini 

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote muandaaji na muhusika mkuu wa filamu hiyo Salum Salehe(man fizo) amesema filamu hiyo ameitengeneza visiwani Zanzibar na imeghalimu dora 13799.45 sawa na zaidi ya milioni 30 kwa madafu ya kibongo

 Aidha amesema wahusika wote wameonesha uwezo mkubwa kwenye nafasi zao jambo lilifanyanya muongozaji asipate shida sana kuwaongoaza "kwenye filamu hii wahusika ni mimi mwenyewe,Mwanaheri,Careen,Deus,Kupa pamoja na Mzee Majuto,ni hadithi ambayo kila mtu ataipenda itakapo kuwa madukani msikose"

 Filamu ya siri ya moyo inatarajia kuingia sokoni tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2016 na inasambazwa na kampuni ya Steps entertainment.