Showing posts with label bongo actress. Show all posts
Showing posts with label bongo actress. Show all posts

Wednesday, March 19, 2014

WASTARA:Sijawai na sitawai kutoa rushwa ya ngono ili nicheze filamu

Mcheza filamu mwenye jina kubwa Wastara Juma amesema ajawai na hawezi kutoa rushwa ya ngono ili acheze filamu

Wastara amesema mtu kutakwa kimapenzi sehemu yoyote ya kazi siku hizi ni jambo la kawiada lakini kwa upande wake hawezi kutoa rushwa ya ngono na haitakuja kutokea

“Mimi siwezi kutoa rushwa ya ngono popote kwanza hiyo ilo wazo sina kichwani mwangu kabisa na siwezi“

Wastara amewataka mabinti wenye vipaji wasiwe na tamaa za kutaka mafanikio kwa halaka mpaka wanafikia atua ya kuuza utu wao kwa kutoa rushwa ya ngojo badala yake wajitume tu kama hipo hipo

SHAMSA FORD:POMBE IMENIZEESHA

DIVA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford,
amefunguka kuwa ameamua kuacha pombe kwa
sababu ameona haina faida yoyote kwake zaidi ya
kumzeesha na kumfanya aonekane kama mama
mtu mzima

Tuesday, March 18, 2014

Wastara:sitakaa ni sahau siku aliyokufa baba wa taifa kwasababu ndio siku niliyoanza kuigiza rasmi

Mcheza filamu mwenye jina kubwa bongo Wastara Juma amesema siku aliyokufa baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere ndio siku aliyoanza kuigiza hivyo awezi kuhisahau siku hiyo kwenye maisha.yake

Amesema mchezo wake wakwanza alicheza na mzee Majuto uliitwa utaishia kunawa na kwamba hapo ndio ikawa mwanzo wa safari yake kwenye tasnia ya filamu

“Mchezo wangu wakwanza ni utaishia kunawa niliocheza na mzee majuto na weza kusema yeye aliona uwezo wangu kwa wakati ule mpaka.sasa na muheshimu sana“

Wastara mpaka sasa anajumla ya filamu zisizopungua 20 uku filamu yake mpya ya Shaymaa ikiendelea kufanya vizuri sokoni hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpaya inayoitwa ‘Last decision‘alikwa na Hemedy Sukeiman na wasanii wengine wengi

Cheki muonekano mpya wa Wema Sepetu baada ya kunyoa

Hizi ni baadhi ya picha za mchezak filamu Wema Sepetu alizoweka instagram zikimuonesha akiwa amenyoa kipara na mashabiki kuanza kumpa sifa kuwa amependeza

Amanda Poshy:ile habari ya uongo kuhusu mimi kubakwa imenipotezea furaha yangu ya maisha

Baada ya habari za uvumi kuwa mcheza filamu Amanda Poshy amebakwa,Amanda amekanusha na kusema hajawai kubakwa kwenye maisha yake na hiyo taarifa imemuumiza sana kwenye maisha yake

“Ni habari mbaya sana kwenye maisha yangu na watu walionisingizia wameniumiza sana

Ni habari ambayo imeumiza mpaka mashabiki wangu wa nje ya nchi wote wanapiga simu wanalaani hiyo habari wengine ata siwajui na sijui wanapata wapi namba zangua ila nashukuru mungu nikiwaelewesha wanaelewa“

Wolper:Lazima nitaolewa nje ya nchi

STAA wa filamu za Kibongo , Jacqueline
Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya
kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya
nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini
mastaa.
, Wolper alisema,
amefikia uamuzi huo kwa sababu ana
uchungu moyoni unaotokana na dhana
waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu
yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo
kuwashusha thamani.
“ Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama
chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa
kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini
kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko
nje.
“ Kule bwana (hajataja nchi ) mtu akimuoa
staa, anampa kipaumbele . Anaweza hata
kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa
na maisha ya mke wake yanakuwa yenye
amani lakini hapa kwetu tunadharaulika
sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu , ”
alisema Wolper na kuongeza :
“ Unajua Watanzania wanaamini staa
kuandikwa magazetini ni uhuni lakini
wanasahau kuwa maisha yake na magazeti
ni kitu cha kawaida kwa sababu ya
kujulikana . Mimi sina haja ya kueleza sana
lakini naapa kabisa , mimi siwezi kuolewa na
Mbongo.

Saturday, March 15, 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU KUBAKWA KWA AMANDA POSH

MAMBO hadharani! Staa wa sinema za
Kibongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’
ameanika ukweli juu ya skendo iliyoenea
kama moto wa kifuu kuwa amebakwa jijini
Arusha.
Staa wa sinema za Kibongo, Tamrina
Mohamed Poshi ‘Amanda’.
Awali, Risasi Jumamosi lilipokea skendo hiyo
kutoka kwa vyanzo vyake ambapo ilidaiwa
kwamba Amanda alifanyiwa ‘unyambilisi’ huo
baada ya kudanganywa kuwa anakwenda
kucheza filamu ya ‘madogo’ fulani wa jijini
humo.
“Mwanzoni nasikia walihitilafiana kwenye
malipo. Amanda alitaka Sh. milioni 2 lakini
baadaye walikubaliana laki 8.
“Kweli Amanda alipofika Arusha alipokelewa
vizuri na kupelekwa hotelini.
“Nasikia baadaye wale jamaa walimuibukia
hotelini wakiwa watatu wakamtisha na
kumbaka kisha wakaingia mitini. Kuna
kipindi magazeti yaliandika anaumwa,”
kilidai chanzo chetu na kuingia mitini.
Baada ya mzigo huo kutua kwenye Dawati la
Risasi Jumamosi , Amanda aliwekwa ‘mtu
kati’ ndipo akaeleza anachokijua juu ya
sakata hilo.
Amanda: “Huo ni uzushi uliotengenezwa na
kijana aliyenipigia simu akaniomba nikacheze
filamu yake lakini tulishindwa kuelewana.
“Walitaka nikacheze sehemu ya mhusika
Mkuu kwa laki 4 lakini niliwakatalia
nikaawambia wafanye Sh. milioni 2.
“Walilalama sana wakidai ndiyo kwanza
wanaanza hivyo wangeomba angalau
nicheze vipande vichache. Tulivutana hadi
nikafika Sh. laki 8 lakini walishindwa na
kudai kuwa najiona niko juu hivyo
nitaona.
“Hata kwenye ukurasa wangu wa
Facebook, huyo jamaa amekuwa
akinichafua. Ukweli ni kwamba sijawahi
hata kuonana naye.
“(huku akimpigia simu mama na baba
yake) mara yangu ya mwisho kwenda
Arusha ilikuwa mwaka 2008. Kama
hamuamini muulizeni mama na baba
yangu. Sijawahi kubakwa katika maisha
yangu.”

Monday, March 10, 2014

Wastara Juma ndio mcheza filamu wa kike bongo mwenye ushawishi kama kiongozi

Wastara Juma ndio mcheza filamu wa kike Tanzania mwenye ushawishi kama kiongozi imeelezwa

Hii inatokana na jinsi anavyojituma kwenye kazi zake za sanaa na kuwa karibu na mashabiki wake jambo linalofanya azidi kupendwa kila kukicha

Wakipiga stori baadhi ya mashabiki wake wanasema Wastara ni msanii anaeipenda kazi yake na sio mbaguzi wala hana majivuno yani ni mtu wawaatu

“Unajua wastara ni tofauti na wasanii wengine yani pamoja nakua kwenye game kwa miaka mingi bado ashuki samani kila msanii anatamani kufanya nae kazi“

NORA ATESWA NA MATAPELI

MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’
amefunguka kuwa anakerwa na matapeli
walioibuka ambao wanawatapeli wasanii wa kike
wakiwadanganya kwamba wanawachezesha
filamu kumbe ‘changa la macho’.

Akistorisha na paparazi wetu, Nora alisema hivi
karibuni alikutwa na mkasa huo baada ya
kupigiwa simu na wanaume wawili waliodai
kwamba wana filamu yao hivyo wanataka
wamchezeshe kama mhusika mkuu (main
character) lakini baada ya kukutana nao,
mazungumzo yao yalikuwa tofauti.
“Walinikera sana, waliniambia kwamba wanataka
kunichezesha filamu lakini nilipoenda kuonana
nao walibadili mazungumzo na kuanza kunitaka
kimapenzi, ujinga mtupu, niliwakatalia,” alisema
Nora.

Saturday, March 08, 2014

WOLPER ACHOMOA SKENDO YA KUTELEKEZA WAZAZI

Staa wa sinema za Kibongo , Jacqueline
Wolper amechomoa madai yaliyoibuka kuwa
hawajali wazazi wake . Baada ya taarifa hizo
za chinichini kuzagaa , Wolper aliibuka na
kuzikanusha:
“ Wazazi wangu ni matajiri kwa pesa gani
nyingi nilizonazo za uwafikia wao kiasi cha
kuwapa matunzo, bado nawategemea hivyo
wanaodai nimetelekeza wazazi ni waongo
tu.”

DAVINA AMSHAURI WASTARA

BAADA ya staa wa filamu za Kibongo ,
Wastara Juma kutoa shukurani kwa wasanii
wenzake zilizotafsiriwa kama anajitabiria
kifo chake , msanii mwenzake , Halima
Yahaya ‘ Davina’ ameibuka na kumtaka
asikate tamaa .
Halima Yahaya ‘ Davina ’ .
Alisema alishtuka baada ya kuona maelezo
gazetini ( Ijumaa Wikienda) ambayo Wastara
alimpongeza kama rafiki mwenye mchango
na hakujua kama anathamini na kukumbuka
vitu watu walivyomfanyia ila kikubwa
amemtaka asikate tamaa kwa yote
yaliyomtokea.
“ Asikate tama , mitihani tumeumbiwa
wanadamu, tunapaswa kuishinda, ” alisema
Davina.

Friday, February 28, 2014

LULU AANIKA MCHECHETO KIZIMBANI

STAA wa sinema za Kibongo , Elizabeth
Michael ‘ Lulu ’ amefunguka kuwa siku
alipokuwa mahakamani akisomewa kesi
inayomkabili ya kumuua bila kukusudia
msanii mwenzake, marehemu Steven
Kanumba, alipata mchecheto sana .

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, siku
hiyo wakati kesi ikiendelea , alipata
mchecheto kiaina na kujikuta ghafla akiwaza
juu ya hatima yake hivyo kuangukia katika
lindi la hofu .
“ Daah ! Nilipata mchecheto ghafla hata sijui
kwa nini , nilivuta picha ya mbali sana na
kujikuta nikijiuliza maswali mengi
yasiyokuwa na majibu , ” alisema .
Msanii huyo alisomewa shitaka lake hilo
Februari 17 , mwaka huu kwenye Mahakama
Kuu, jijini Dar, kesi hiyo iliahirishwa hadi
itakapotajwa tena baada ya msanii huyo
kujibu maswali ya kweli au si kweli .

BABY MADAHA:SHILOLE MCHEZA VIGODORO

MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby
Joseph ‘ Madaha ’ amemchana staa
mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole ’ kwa
kumwambia ni mcheza muziki wa uswahilini
(vigodoro) .

Kauli hiyo ya msanii huyo anayetamba na
Wimbo wa Summer Holyday , ameitoa siku
chache baada Shilole kutema cheche zake
kuwa Madaha aache kumfuatilia kwani
amekuwa akiingia kwenye anga zake mara

“ Hivi huyu ana akili au matope ,
nimfuatefuate ana nini ? Hebu aangalie
muziki wangu ninaopiga na wake . Yeye ni
wa hapa hapa, mcheza vigodoro, ”
alifunguka Madaha

KAJALA MASANJA ANYWESHWA SUMU

STAA wa sinema za Kibongo , Kajala Masanja
amejikuta katika hali mbaya kufuatia
kunyweshwa sumu na mtu ambaye
hakuweza kufahamika mara moja .
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita
maeneo ya Tegeta jijini Dar katika Klabu ya
Seventy One ambayo alikwenda kujiachia na
marafiki zake .
Chanzo cha uhakika , kilipenyeza habari
kuwa, Kajala alinyweshwa sumu hiyo kupitia
kwenye glasi ambayo aliwekewa juisi
ambapo haikuweza kufahamika mara moja
kuwa aliwekewa kabla au baada ya
mhudumu kumpa huduma .
“ Unajua mambo ya klabu tena, kila mtu
alikuwa bize na mambo yake , hivyo
hatukuweza kugundua mara moja kuwa nani
alihusika, lakini tulishangaa ghafla Kajala
alijisikia vibaya hivyo marafiki zake wa
karibu walimkimbiza nyumbani kwao kisha
hospitali , ” kilisema chanzo hicho

Wednesday, February 26, 2014

VAI WA UKWELI:TAMAA YA FEDHA ILINIPONZA,NAJUTA

SIKU chache baada ya msanii anayekuja
kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za
Kibongo, Isabela Francis ‘ Vai wa Ukweli ’
kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa
kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua
Maovu ‘ OFM ’ , ameibuka na kusema ,
anajuta , amekoma na hatarudia tena.

Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa
kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na
hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita , ambapo
msanii huyo aliingia mkenge baada ya
kukubali kukutana na ‘pedeshee ’ mmoja
kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda
kwa malipo ya shilingi 500, 000.
Vai alivyonaswa akiwa mawindoni.
Akizungumza  juzi ,
Jumatatu jijini Dar es Salaam , Vai alisema:
“ Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini
pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba
ndugu zangu na mashabiki wangu wote
wanisamehe kwa dhati kabisa .

Monday, February 24, 2014

LULU ADAIWA KUKUWADIWA NA STEVEN NYERERE

OOHOOO! Elizabeth Michael ‘ Lulu ’ amekwaa
skendo ya kudaiwa kukuwadiwa na
mwigizaji mwenzake , Steven Mengere ‘ Steve
Nyerere’ kwa mwanaume anayedaiwa
kutoka naye kimapenzi kwa sasa anayetajwa
kwa jina moja la Johnson .

Chanzo makini kilipenyeza ‘ upupu’ huo
ambao umefafanuliwa na Steve Nyerere
kuwa ukaribu wa Lulu na bosi huyo
umetokana na kazi kwani yeye na Lulu
wameingia mkataba hivyo walitegemea
kusikia manenomaneno .
Lulu alipotafutwa kuhusiana na ishu hiyo,
alitiririka: “ Wabongo wanapenda sana
kuzusha mambo , sijawahi kuwa na
mwanaume anayeitwa Johnson zaidi ya
kuwa bosi wangu .

BUNGE LA KATIBA;MWAKIFWAMBA,BATULI WAKWAA SKENDO

WAKATI mchakato wa Bunge la Katiba
ukianza leo mjini Dodoma , ishu hiyo
imemtia kwenye tope Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania ( TAFF ), Simon
Mwakifwamba baada ya kukwaa skendo ya
‘kutoka ’ na mwigizaji Yobnesh Yusuph
‘Batuli ’ walipotimba mkoani humo .
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’ .
Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye
aliachwa katika safari hiyo ya kwenda
kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye
mchakato wa katiba mpya, Mwakifwamba
alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma
kwa sababu hakuwa na vigezo.
“ Akina Monalisa ( Yvone - Cherry Ngatikwa )
walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani,
sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa
changanya na zako, ” alisema msanii huyo .
Akizungumzia skendo hiyo , Mwakifwamba
alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo
anajua nyuma yake kuna kundi
linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni
kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo .
“ Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je,
akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo
hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri
kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo .
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
( TAFF) , Simon Mwakifwamba .
Kwa upande wake Batuli alifunguka : “ Si
kweli bwana , wameshatuzushia mambo
kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara
sijui nini …sasa naona wamekuja na hili la
mapenzi. Wabongo tuache majungu.
Katika safari ya Dodoma , mbali na Monalisa ,
wawili hao waliambatana na wasanii
wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo
Dude, John Kitime , P - Funk Majani na Abdul
Salvador ambapo ndani ya bunge hilo
linalotarajiwa kutikisa , wanawakilishwa na
Paul Mtendah

Sunday, February 23, 2014

SHAMSA APIGWA NDOA YA KIMILA

WAKATI wadau wa filamu za Kibongo
wakisubiri kwa hamu kushuhudia ndoa ya
staa wao , Shamsa Ford imebainika kwamba
msanii huyo ameshapigwa ndoa ya
kimyakimya na mchumba wake wa muda
mrefu ambaye pia ni mzazi mwenzake ,
Dickson ‘ Dick ’.
Shamsa Ford .
Kwa mujibu wa chanzo makini , wawili hao
wanadaiwa kufunga ndoa ya kimila
nyumbani kwa mwanaume huyo , Tarime
mkoani Mara wiki kadhaa zilizopita .
“ Shamsa na Dick tayari wamefunga ndoa ya
kimila kijijini kwa mwanaume Tarime
ambapo walichinjiwa mbuzi na kufanyiwa
mambo mbalimbali ya kimila lakini wenyewe
wanafanya siri, ” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo , paparazi
wetu alimtafuta Shamsa ili kupata ukweli
wa habari hizo na staa huyo alikiri kufunga
ndoa ya kimila na Dick na sasa wanaishi
kama mke na mume.
“ Ni kweli tumefunga ndoa ya kimila,
tukachinjiwa mbuzi na kufanyiwa mambo ya
mila ya upande wa mume wangu , ndoa ya
kidini itakuwa ni sapraiz lakini kwa sasa
sizungumzii tena mambo hayo , ” alisema
Shamsa

Saturday, February 22, 2014

AUNT EZEKIEL AANGUKA KWA PRESHA,ALAZWA

STAA wa filamu za Kibongo , Aunt Ezekiel
amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kuanguka ghafla kwa presha akiwa ‘ location ’
jijini Tanga ,

Staa wa filamu za Kibongo , Aunt Ezekiel .
Kwa mujibu wa chanzo, Aunt akiwa katika
harakati za kuigiza filamu anayocheza na
Amri Athuman ‘ Mzee Majuto ’, ghafla
alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya
Gesha jijini humo .

Baada ya kuzipata habari hizi , mapaparazi
wetu walimtafuta Aunt kwa njia ya simu na
alipopatikana alikiri kuanguka kutokana na
kusumbuliwa na presha ya kushuka .
“ Kweli nilikuwa shutting na Mzee Majuto ,
ghafla nilianguka na kukimbizwa hospitali ,
wameniwekea dripu mkononi ila
namshukuru Mungu , naendelea vizuri , ”
alisema Aunt