Friday, February 28, 2014

KAJALA MASANJA ANYWESHWA SUMU

STAA wa sinema za Kibongo , Kajala Masanja
amejikuta katika hali mbaya kufuatia
kunyweshwa sumu na mtu ambaye
hakuweza kufahamika mara moja .
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita
maeneo ya Tegeta jijini Dar katika Klabu ya
Seventy One ambayo alikwenda kujiachia na
marafiki zake .
Chanzo cha uhakika , kilipenyeza habari
kuwa, Kajala alinyweshwa sumu hiyo kupitia
kwenye glasi ambayo aliwekewa juisi
ambapo haikuweza kufahamika mara moja
kuwa aliwekewa kabla au baada ya
mhudumu kumpa huduma .
“ Unajua mambo ya klabu tena, kila mtu
alikuwa bize na mambo yake , hivyo
hatukuweza kugundua mara moja kuwa nani
alihusika, lakini tulishangaa ghafla Kajala
alijisikia vibaya hivyo marafiki zake wa
karibu walimkimbiza nyumbani kwao kisha
hospitali , ” kilisema chanzo hicho

No comments:

Post a Comment