Wednesday, February 26, 2014

VAI WA UKWELI:TAMAA YA FEDHA ILINIPONZA,NAJUTA

SIKU chache baada ya msanii anayekuja
kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za
Kibongo, Isabela Francis ‘ Vai wa Ukweli ’
kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa
kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua
Maovu ‘ OFM ’ , ameibuka na kusema ,
anajuta , amekoma na hatarudia tena.

Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa
kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na
hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita , ambapo
msanii huyo aliingia mkenge baada ya
kukubali kukutana na ‘pedeshee ’ mmoja
kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda
kwa malipo ya shilingi 500, 000.
Vai alivyonaswa akiwa mawindoni.
Akizungumza  juzi ,
Jumatatu jijini Dar es Salaam , Vai alisema:
“ Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini
pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba
ndugu zangu na mashabiki wangu wote
wanisamehe kwa dhati kabisa .

No comments:

Post a Comment