STAA wa filamu za Kibongo , Jacqueline
Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya
kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya
nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini
mastaa.
, Wolper alisema,
amefikia uamuzi huo kwa sababu ana
uchungu moyoni unaotokana na dhana
waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu
yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo
kuwashusha thamani.
“ Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama
chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa
kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini
kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko
nje.
“ Kule bwana (hajataja nchi ) mtu akimuoa
staa, anampa kipaumbele . Anaweza hata
kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa
na maisha ya mke wake yanakuwa yenye
amani lakini hapa kwetu tunadharaulika
sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu , ”
alisema Wolper na kuongeza :
“ Unajua Watanzania wanaamini staa
kuandikwa magazetini ni uhuni lakini
wanasahau kuwa maisha yake na magazeti
ni kitu cha kawaida kwa sababu ya
kujulikana . Mimi sina haja ya kueleza sana
lakini naapa kabisa , mimi siwezi kuolewa na
Mbongo.
Tuesday, March 18, 2014
Wolper:Lazima nitaolewa nje ya nchi
Labels:
bongo actress
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment