Monday, February 24, 2014

BUNGE LA KATIBA;MWAKIFWAMBA,BATULI WAKWAA SKENDO

WAKATI mchakato wa Bunge la Katiba
ukianza leo mjini Dodoma , ishu hiyo
imemtia kwenye tope Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania ( TAFF ), Simon
Mwakifwamba baada ya kukwaa skendo ya
‘kutoka ’ na mwigizaji Yobnesh Yusuph
‘Batuli ’ walipotimba mkoani humo .
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’ .
Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye
aliachwa katika safari hiyo ya kwenda
kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye
mchakato wa katiba mpya, Mwakifwamba
alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma
kwa sababu hakuwa na vigezo.
“ Akina Monalisa ( Yvone - Cherry Ngatikwa )
walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani,
sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa
changanya na zako, ” alisema msanii huyo .
Akizungumzia skendo hiyo , Mwakifwamba
alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo
anajua nyuma yake kuna kundi
linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni
kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo .
“ Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je,
akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo
hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri
kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo .
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
( TAFF) , Simon Mwakifwamba .
Kwa upande wake Batuli alifunguka : “ Si
kweli bwana , wameshatuzushia mambo
kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara
sijui nini …sasa naona wamekuja na hili la
mapenzi. Wabongo tuache majungu.
Katika safari ya Dodoma , mbali na Monalisa ,
wawili hao waliambatana na wasanii
wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo
Dude, John Kitime , P - Funk Majani na Abdul
Salvador ambapo ndani ya bunge hilo
linalotarajiwa kutikisa , wanawakilishwa na
Paul Mtendah

No comments:

Post a Comment