Saturday, March 15, 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU KUBAKWA KWA AMANDA POSH

MAMBO hadharani! Staa wa sinema za
Kibongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’
ameanika ukweli juu ya skendo iliyoenea
kama moto wa kifuu kuwa amebakwa jijini
Arusha.
Staa wa sinema za Kibongo, Tamrina
Mohamed Poshi ‘Amanda’.
Awali, Risasi Jumamosi lilipokea skendo hiyo
kutoka kwa vyanzo vyake ambapo ilidaiwa
kwamba Amanda alifanyiwa ‘unyambilisi’ huo
baada ya kudanganywa kuwa anakwenda
kucheza filamu ya ‘madogo’ fulani wa jijini
humo.
“Mwanzoni nasikia walihitilafiana kwenye
malipo. Amanda alitaka Sh. milioni 2 lakini
baadaye walikubaliana laki 8.
“Kweli Amanda alipofika Arusha alipokelewa
vizuri na kupelekwa hotelini.
“Nasikia baadaye wale jamaa walimuibukia
hotelini wakiwa watatu wakamtisha na
kumbaka kisha wakaingia mitini. Kuna
kipindi magazeti yaliandika anaumwa,”
kilidai chanzo chetu na kuingia mitini.
Baada ya mzigo huo kutua kwenye Dawati la
Risasi Jumamosi , Amanda aliwekwa ‘mtu
kati’ ndipo akaeleza anachokijua juu ya
sakata hilo.
Amanda: “Huo ni uzushi uliotengenezwa na
kijana aliyenipigia simu akaniomba nikacheze
filamu yake lakini tulishindwa kuelewana.
“Walitaka nikacheze sehemu ya mhusika
Mkuu kwa laki 4 lakini niliwakatalia
nikaawambia wafanye Sh. milioni 2.
“Walilalama sana wakidai ndiyo kwanza
wanaanza hivyo wangeomba angalau
nicheze vipande vichache. Tulivutana hadi
nikafika Sh. laki 8 lakini walishindwa na
kudai kuwa najiona niko juu hivyo
nitaona.
“Hata kwenye ukurasa wangu wa
Facebook, huyo jamaa amekuwa
akinichafua. Ukweli ni kwamba sijawahi
hata kuonana naye.
“(huku akimpigia simu mama na baba
yake) mara yangu ya mwisho kwenda
Arusha ilikuwa mwaka 2008. Kama
hamuamini muulizeni mama na baba
yangu. Sijawahi kubakwa katika maisha
yangu.”

No comments:

Post a Comment