Saturday, February 22, 2014

AUNT EZEKIEL AANGUKA KWA PRESHA,ALAZWA

STAA wa filamu za Kibongo , Aunt Ezekiel
amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kuanguka ghafla kwa presha akiwa ‘ location ’
jijini Tanga ,

Staa wa filamu za Kibongo , Aunt Ezekiel .
Kwa mujibu wa chanzo, Aunt akiwa katika
harakati za kuigiza filamu anayocheza na
Amri Athuman ‘ Mzee Majuto ’, ghafla
alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya
Gesha jijini humo .

Baada ya kuzipata habari hizi , mapaparazi
wetu walimtafuta Aunt kwa njia ya simu na
alipopatikana alikiri kuanguka kutokana na
kusumbuliwa na presha ya kushuka .
“ Kweli nilikuwa shutting na Mzee Majuto ,
ghafla nilianguka na kukimbizwa hospitali ,
wameniwekea dripu mkononi ila
namshukuru Mungu , naendelea vizuri , ”
alisema Aunt

No comments:

Post a Comment