WAKATI wadau wa filamu za Kibongo
wakisubiri kwa hamu kushuhudia ndoa ya
staa wao , Shamsa Ford imebainika kwamba
msanii huyo ameshapigwa ndoa ya
kimyakimya na mchumba wake wa muda
mrefu ambaye pia ni mzazi mwenzake ,
Dickson ‘ Dick ’.
Shamsa Ford .
Kwa mujibu wa chanzo makini , wawili hao
wanadaiwa kufunga ndoa ya kimila
nyumbani kwa mwanaume huyo , Tarime
mkoani Mara wiki kadhaa zilizopita .
“ Shamsa na Dick tayari wamefunga ndoa ya
kimila kijijini kwa mwanaume Tarime
ambapo walichinjiwa mbuzi na kufanyiwa
mambo mbalimbali ya kimila lakini wenyewe
wanafanya siri, ” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo , paparazi
wetu alimtafuta Shamsa ili kupata ukweli
wa habari hizo na staa huyo alikiri kufunga
ndoa ya kimila na Dick na sasa wanaishi
kama mke na mume.
“ Ni kweli tumefunga ndoa ya kimila,
tukachinjiwa mbuzi na kufanyiwa mambo ya
mila ya upande wa mume wangu , ndoa ya
kidini itakuwa ni sapraiz lakini kwa sasa
sizungumzii tena mambo hayo , ” alisema
Shamsa
Sunday, February 23, 2014
SHAMSA APIGWA NDOA YA KIMILA
Labels:
bongo actress
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment