Monday, March 10, 2014

NORA ATESWA NA MATAPELI

MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’
amefunguka kuwa anakerwa na matapeli
walioibuka ambao wanawatapeli wasanii wa kike
wakiwadanganya kwamba wanawachezesha
filamu kumbe ‘changa la macho’.

Akistorisha na paparazi wetu, Nora alisema hivi
karibuni alikutwa na mkasa huo baada ya
kupigiwa simu na wanaume wawili waliodai
kwamba wana filamu yao hivyo wanataka
wamchezeshe kama mhusika mkuu (main
character) lakini baada ya kukutana nao,
mazungumzo yao yalikuwa tofauti.
“Walinikera sana, waliniambia kwamba wanataka
kunichezesha filamu lakini nilipoenda kuonana
nao walibadili mazungumzo na kuanza kunitaka
kimapenzi, ujinga mtupu, niliwakatalia,” alisema
Nora.

No comments:

Post a Comment