Friday, February 28, 2014

LULU AANIKA MCHECHETO KIZIMBANI

STAA wa sinema za Kibongo , Elizabeth
Michael ‘ Lulu ’ amefunguka kuwa siku
alipokuwa mahakamani akisomewa kesi
inayomkabili ya kumuua bila kukusudia
msanii mwenzake, marehemu Steven
Kanumba, alipata mchecheto sana .

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, siku
hiyo wakati kesi ikiendelea , alipata
mchecheto kiaina na kujikuta ghafla akiwaza
juu ya hatima yake hivyo kuangukia katika
lindi la hofu .
“ Daah ! Nilipata mchecheto ghafla hata sijui
kwa nini , nilivuta picha ya mbali sana na
kujikuta nikijiuliza maswali mengi
yasiyokuwa na majibu , ” alisema .
Msanii huyo alisomewa shitaka lake hilo
Februari 17 , mwaka huu kwenye Mahakama
Kuu, jijini Dar, kesi hiyo iliahirishwa hadi
itakapotajwa tena baada ya msanii huyo
kujibu maswali ya kweli au si kweli .

No comments:

Post a Comment