Showing posts with label new movie. Show all posts
Showing posts with label new movie. Show all posts

Saturday, December 07, 2013

Shaymaa ya wastara yapokelewa mtaani

Baada ya muda mrefu kupita atimae filamu ya Wastara Sajuki imeingia mtaani rasmi jana

Kupitia ukurasa wake facebook ameposti picha akiwa ameashika filamu hiyo mkononi na baada ya muda mashabiki wake wakaanza kumtumia picha wakiwa wameshika filamu hiyo

Shaymaa inasambazwa na kampuni ya steps na ndani ikiwa imewashirikisha mastaa wengine kama Salm Jabu na Yusuph Mlela

Thursday, December 05, 2013

Riyama:king‘amuzi ni funzo kwa wanaume wenye wivu na wachoyo wa chakula

Muigizaji nyota wa filamu nchini Riyama Ally amewataka wapenzi wa wakazi zake kuinunua filamu ya mpya king‘amuzi ili wajifunze njinsi ya kuishi na mwanaume mwenye wivu na uchoyo wa chakula

“Filamu ya King'amuzi imetokana ipo madukani inahusu mwanaume ana wivu wakupitiliza na uchoyo wachakula naomba wapenzi na mashabiki wangu wainunue naamini watajifunza kitu“

Hii ndio filamu mpya ya Baby Madaha inaitwa Gal Bladder

Filamu hii inahusu kisa cha mwanadada Bahati (Baby Madaha) ambaye alipewa kazi ya ndani na bosi wake lakini boss alimgeuka na kuanza kumbaka na kumtesa bila huruma.

Baada ya mateso kuzidi aliamua kutiroka na kuanzisha kikundi chake cha kisasi kilichokuwa kwa wote wenye tabia hizo.

Ni filamu ya kipekee na ya tofauti katika soko la bongo. Inatarajiwa kutoka hivi karibuni. Hii si ya kukosa hata kidogo.

Bongo movie

Tuesday, December 03, 2013

IRENE PAUL:Haikuwa rahisi kuigiza kama changudoa kwenye filamu ya shujaa

Muigizaji wa filamu nchini, Irene Paul amesema haikuwa rahisi kuigiza kama changudoa (msichana anayejiuza mwili) kwenye filamu kuhusu masuala ya Ukimwi, Shujaa.

Akiongea na mtandao wa Bongo5, Irene alisema hajawahi kufanya filamu ya aina hiyo lakini alipofuatwa kuigiza hakusita kukubali kwakuwa alitaka kuonesha utofauti katika uigizaji wake.

Hata hivyo aliongeza kuwa wakati wa kushoot filamu hiyo mtaani watu wengi walihisi kweli ni changudoa.

“Changamoto zilikuwa nyingi sana. kuna sehemu zingine nilikuwa ninasimama katika movie na watu walifikiri mimi ni changudoa wa ukweli kulingana na nguo na kila kitu,” alisema.
 
“Ilichukua muda wa ziada kufanya vitu ambavyo vitanifanya nionekane tofauti ndio maana mpaka Zamaradi aliweza kunitofautisha mimi uchangudoa wangu na uchangudoa wa mtu mwingine.”

Bongo 5

WASTARA:Kwenye filamu ya Shaymaa nimbadilisha Mlela

Mcheza filamu mwenye heshima ya juu bongo movie Wastara SaJuki amesema kwenye filamu yake mpya ya Shaymaa amembadilisha muingizaji mwenzie Yusuph Mlele kwa kumpa nafasi ya kucheza kama baba wa familia.

Akipiga stori na blog hii Wastara amesema filamu nyingi Mlela amekua akicheza nafasi tofauti na za baba wa familia ndio maana akampa nafasi hiyo aoneshe uwezo wake zaidi.

“Nimembadili Mlela kacheza kama mume wangu kwenye filamu ya shaymaa“

Amesema filamu hiyo inahusu wasichana wawili waliofanana karibu kila kitu mpaka majina na inatarajia kuingia sokoni ijumaa ya.wiki hii

Monday, December 02, 2013

WASTARA:Filamu yangu mpya ya Shaymaa nifunzo kwa watanzania waliopoteza matumaini

Msanii wa filamu nchini Wastara Sajuki amesema filamu yake mpya ya Shaymaa ni funzo kwa watanzania waliopoteza matumaini kwenye maisha

Filamu hiyo aliyowashilikisha Yusuph Mlela na Salma Jabu inahusu wasichana wawili waliofanana karibu kila kitu mpaka majina

“shaymaa maana yake ni alama na inazungumzia wasichana wawili waliofanana kila kitu mpaka majina Nisha amecheza kama Shaymaa na mimi nimecheza kama Shaymaa zaidi mtaona filamu“

Filamu ya Shaymaa inatarijia kuingia sokono tarehe sita mwezi huu na inasambazwa na steps.

Friday, November 29, 2013

Filamu ya Shaymaa kutoka tarehe 6 mwezi ujao

Filamu mpya ya Wastara Sajuki inayokwenda kwa jina la Shaymaa inatarajia kuingia mtaani tarehe 6 mwezi ujao

Filamu hiyo imewshirikisha waigizaji wengi akiwemo Salma Jabu Nisha na Yosuph Mlela

Thursday, November 28, 2013

Soma alichoandika mwanamuziki Zola D kwenye akaunti yake ya facebook

“inshallah soon nitaanza kushot movie yangu ya kwanza ya actions inaitwa
( mr police man),ni bonge la movie mapigo ya kufa mtu na bonge la story watu wangu i qwrty hd video na sound za kisasa nipeni surport watu wangu tuonyeshe kimataifa kama tunaweza tukacheze holwood huko“

Filamu ya Uaminifu Dhaifu ya Bondi imemalizika kufanyiwa shooting tazama baadhi ya picha za location

Sunday, November 24, 2013

MAJUTO yawakutanisha Salma Nisha na lrene Paul

Kwa mara ya kwanza mastaa wa wili wa filamu za kibongo Irene Paul na Salma Nisha wakutana ndani ya filamu ya Majuto.

Filamu hiyo ni ya pili kutoka kwenye kampuni ya krema inayomilikiwa na Irene na inaelezea maisha halisi ya mtanzania.

Filamu hii imetoka jana pata nakala yako huone walichokifanya mastaa hawa.

Saturday, November 23, 2013

Wastara:new movie ni mtihani nafanya nisio wai kuyafanya

Wastara Sajuki amewomba watanzania wasimchulie tofauti wakiona amevaa nguo fupi kwenye filamu maana filamu sio maisha halisi

Amesema kazi zote zinazofata sasa za kushirikishwa amepangiwa kuvaa mavazi ambayo ajawi kuyavaa

“new movie ni mtihani nafanya nisiyowahi kufanya navaa nisivyowahi kuvaa but is my job no option gud movie mtajifunza mengi kuipitia filamu hii ya UAMINIFU DHAIFU from Director BOND BIN SINAN mtunzi uBOND BIN SINAN“

Wednesday, November 20, 2013

Linex:Mzee Majuto anakipaji sio ambacho sio cha kawaida

Msanii mwenye sauti yenye hisia za juu Linex Sunday ameonesha furaha yake baada ya kukutana na Mzee Majuto kwenye filam mpya inayoitwa Mwajuma na iki ndio ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook

“Hii ni mwa mala ya kwanza nakutana na Mr Been wa Tz Mzee Majuto jana Location#Mwajuma nipe#Movie#Ki ukweli yule Mzee kabarikiwa kipaji ambacho sio cha kawaida some time nilikua nashindwa kuigiza nabaki nacheka tu#wetheVoa“