Muigizaji wa filamu nchini, Irene Paul amesema haikuwa rahisi kuigiza kama changudoa (msichana anayejiuza mwili) kwenye filamu kuhusu masuala ya Ukimwi, Shujaa.
Akiongea na mtandao wa Bongo5, Irene alisema hajawahi kufanya filamu ya aina hiyo lakini alipofuatwa kuigiza hakusita kukubali kwakuwa alitaka kuonesha utofauti katika uigizaji wake.
Hata hivyo aliongeza kuwa wakati wa kushoot filamu hiyo mtaani watu wengi walihisi kweli ni changudoa.
“Changamoto zilikuwa nyingi sana. kuna sehemu zingine nilikuwa ninasimama katika movie na watu walifikiri mimi ni changudoa wa ukweli kulingana na nguo na kila kitu,” alisema.
“Ilichukua muda wa ziada kufanya vitu ambavyo vitanifanya nionekane tofauti ndio maana mpaka Zamaradi aliweza kunitofautisha mimi uchangudoa wangu na uchangudoa wa mtu mwingine.”
Bongo 5
No comments:
Post a Comment