MAMBO hadharani! Penzi ‘ hoti’ la mastaa
mahiri wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans
na Vincent Kigosi ‘ Ray’ kwa sasa limekuwa
kama la njiwa kwani mara nyingi kila
sehemu wapo pamoja na hakuna kificho
tena.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa mastaa
hao wamekuwa wakionekana pamoja mara
nyingi na hivi sasa inadaiwa kuwa wanaishi
pamoja huku wakiwa na mtoto wa Chuchu
aitwaye Danzel .
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa
kutokana na mapenzi hayo kukolea siku
hadi siku , juzikati baadhi ya ndugu wa
mastaa hao walianza vikao vya chini kwa
chini ili kuhakikisha mwaka huu wasanii hao
wanafunga ndoa lakini haijajulikana kama
watafungia kanisani au msikitini kwa kuwa
wana dini tofauti .
“ Yaani sasa hivi hakuna siri hata chembe, ni
fulu kujiachia. Mara nyingi wapo pamoja kila
sehemu yaani kama njiwa, ” kilisema chanzo
chetu.
Chanzo hicho kilizidi kudai kwamba mara
nyingi Ray na Chuchu wanapenda kwenda
kuogelea na kujiachia kama mke na mume
kwenye hoteli moja maarufu ( jina
linahifadhiwa) iliyoko maeneo ya Mbezi
Beach jijini Dar huku wakijifotoa picha za
kumbukumbu.
Baada ya kujazwa ‘ info’ hizo na kumwagiwa
picha za mastaa hao , gazeti hili lilimtafuta
Chuchu kisha kumuuliza kuhusiana na penzi
lake na Ray kuwa ‘ shatashata ’ ambapo
alifunguka kuwa kama kuna mtu anawaona
wakiwa pamoja ni kwa sababu hivi sasa eti
wanaandaa ‘ sinema ’ yao wawili.
Alipotafutwa Ray ili kuulizwa kuhusiana na
ishu hiyo , simu yake ilikuwa ikiita bila
kupokelewa kwa muda wa nusu saa
No comments:
Post a Comment