Akizungumzia filamu hiyo hapo jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.
"Napenda sana kusikiliza maoni ya mashabiki zangu na kuyafanyia kazi,kwenye filamu ya SHIDA nimewakumbusha Matilda kwa wale walioniomba nitoe serious movie pia sio comedy peke yake.. mimi mwenyewe nililia Ukweli kwa matukio yake, ingawa pia SHIDA
itakuburudisha,kukuelelimisha na kukupa ladha halisi ya maisha ya mtanzania ungana nasi Gabo,Nisha,Tunu na wasanii kibao kutoka Zanzibar house of talent,chini uongozi na wapiga picha mashuhuri Tanzania CLEAR PICTURES"
Alisema mashabiki wategemee mambo mengi mazuri zaidi kutoka kwake, kwani mara nyingi amekuwa akifanya kazi kwa mpangilio ili kuhakikisha anatoa vitu vyenye ubora.
Filamu hii inasambazwa na kampuni ya steps entetainment kuwa wakwanza kuipata kwa kuandika 0788233635
No comments:
Post a Comment