Saturday, December 03, 2016

UZINDUZI WA SIRI YA MOYO WAFANYIKA DAR ES SALAAM











Uzinduzi wa filamu ya Siri ya moyo umefanyika kwenye ukumbi wa sinema Suncrest ulipo ndani ya jumba la biashara,Quality centre na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa filamu nchini 

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote muandaaji na muhusika mkuu wa filamu hiyo Salum Salehe(man fizo) amesema filamu hiyo ameitengeneza visiwani Zanzibar na imeghalimu dora 13799.45 sawa na zaidi ya milioni 30 kwa madafu ya kibongo

 Aidha amesema wahusika wote wameonesha uwezo mkubwa kwenye nafasi zao jambo lilifanyanya muongozaji asipate shida sana kuwaongoaza "kwenye filamu hii wahusika ni mimi mwenyewe,Mwanaheri,Careen,Deus,Kupa pamoja na Mzee Majuto,ni hadithi ambayo kila mtu ataipenda itakapo kuwa madukani msikose"

 Filamu ya siri ya moyo inatarajia kuingia sokoni tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2016 na inasambazwa na kampuni ya Steps entertainment.

No comments:

Post a Comment