Duh! Habari mpya kutoka huko Hong Kong,
China zinaeleza kuwa kama atapatikana na hatia
ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’,
modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff
‘Jack Patrick’ atatumikia kifungo cha miaka kumi
jela.
Jack. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho
kilikwenda kumtembelea Jack akiwa nyuma ya
nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu
Machi mosi, mwaka huu, mwanamitindo huyo
amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka
jela hivi karibuni.
“Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana
matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana
maumivu ya kupitiliza,” kilisema chanzo hicho.
Jack Patrick akiwa akiwa mikononi mwa polisi
nchini China baada ya kukutwa na pipi za
heroin tumboni. Mpashaji huyo alizidi kuweka
wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni
ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi
atakumbana na kifungo, si chini ya miaka kumi,
jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi
kila kukicha huku akituma salamu nyumbani
kwao Bongo.
Jack alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau,
Hong Kong mwezi Desemba, mwaka jana
ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma
Septemba, mwaka huu.
haryeth paul at
Monday, March 10, 2014
JACK PATRICK JELA MIAKA 10 KAMA IKIHIBITIKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment