Saturday, February 08, 2014

LULU KESI UPYAA

KAZI inaanza tena! Supastaa wa filamu za
Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu ’
anapanda katika kizimba cha Mahakama
Kuu ya Tanzania kwa yale madai ya kumuua
bila kukusudia , aliyekuwa nyota wa muvi
nchini , marehemu Steven Charles Kanumba
‘The Great ’, Risasi Jumamosi limeambiwa .
Supastaa wa filamu za Bongo , Elizabeth
Michael Kimemeta ‘ Lulu ’ .
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es
Salaam , mtoa habari ambaye aliomba
hifadhi ya jina alisema kuwa, Februari 17 ,
mwaka huu, staa huyo atatakiwa
mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake
kuanza huku akisema , kuna mabadiliko
kidogo katika kusikilizwa kwa kesi hiyo .
Marehemu Steven Charles Kanumba ‘ The
Great’ .
ITAKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo , Lulu
mwenye umri wa miaka 18, atasomewa
upya mashitaka dhidi yake ambapo
atatakiwa kujibu tena kama anakubali aliua
bila kukusudia au la!
“ Elizabeth ( Lulu ) atasomewa upya mashitaka
ya kumuua Kanumba bila kukusudia .
“ Ataulizwa ni kweli au si kweli? Atatakiwa
kujibu swali moja kati ya hayo mawili, kama
ni kweli atasema kweli kama si kweli
atasema si kweli , ” kilisema chanzo hicho
huku kikisisitiza jina lake lisichorwe gazetini .
MUDA WA KESI SIKU 730
Habari zaidi zikadondokea Dawati la Risasi
Jumamosi na kusema kwamba , kesi hiyo
itaendeshwa kwa siku mia saba na
thelathini (730 ), kwa maana ya miaka miwili
hadi hukumu itakapotolewa .
NI NDANI YA SHERIA MPYA
Katika Siku ya Sheria Duniani
iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam ,
Februari 3 , mwaka huu , Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mohamed Chande Othman
alisema kuanzia sasa kesi zote za jinai
zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha
miaka miwili .
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu
hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016
itatakiwa iwe imemalizika.
Wakili wa Lulu , Peter Kibatala.
WAKILI WAKE
Chanzo hicho kililithibitishia gazeti hili
kwamba , Lulu atatetewa na yuleyule wakili
wake mwenye ‘ ngekewa’ ya kuwatetea watu
maarufu nchini , Peter Kibatala .
Kibatala ameshawahi kuwa wakili wa
Mbongo Fleva , Isaac Waziri Makuto ‘ Lord
Eyez’ katika kesi ya madai ya kuiba ‘ power
window’ za gari la msanii mwingine wa
Bongo Fleva , Omary Faraji Nyembo ‘ Ommy
Dimpoz’ .
Pia aliwahi kumwakilisha wakili mwezake ,
Mabere Nyaucho Marando kwenye kesi ya
Mbongo Fleva , Judith Wambura ‘ Jide ’
alipoburuzwa kortini na uongozi wa Clouds
Media Group baada ya Marando kuwa na
udhuru.
Ilibaki kidogo awe wakili wa Miss Tanzania
2006, Wema Isaac Sepetu katika kesi ya
kumpiga makofi meneja wa hoteli moja ( jina
tunalo ) iliyopo Kawe Beach , Godluck
Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya
shauri hilo kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo
Kawe, Dar.
HAWA HUENDA WAKAITWA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu , katika
kesi hiyo huenda wakaitwa watu ambao
watasaidia kutoa ushahidi .
Watu hao ni wale waliokuwa na ukaribu na
marehemu , hasa siku ya tukio au
kushirikishwa kwa namna moja au nyingine
kwa jinsi ambavyo waendesha mashitaka
wataona.
DOKTA KIDUME
Aliyekuwa akimtibu Kanumba, Dokta Kidume
anaweza kufika mahakamani hapo kwa
sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili kufika
kwenye chumba cha marehemu mara
baada ya kuanguka.
Mdogo’ wa marehemu Kanumba , Seth
Bosco.
SETH BOSCO
Huyu ni ‘ mdogo’ wa marehemu Kanumba,
yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja na
marehemu , ila vyumba tofauti. Ndiye
aliyemwona Kanumba akiwa katika hali
mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na
kukimbia kumwita Dokta Kidume .
Hawa wote walishahojiwa na Jeshi la Polisi
Tanzania katika Kituo cha Oysterbay , Dar,
mara baada ya kifo hicho. Seth alihojiwa
mara tano .
TUJIKUMBUSHE
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012
nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam .
Kifo chake kilidaiwa kilitokana na kuangukia
sehemu ya nyuma ya kichwa na hivyo
kuufanya ubongo kutikisika (brain
concussion).
Hata hivyo, baadaye ilifahamika kuwa,
sehemu ya maini na majimaji ya machoni
vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili
kubaini endapo kulikuwa na sumu au kitu
kingine katika mwili wa Kanumba. Majibu
hayajatoka hadi leo.
WAKILI KIBATALA
Risasi Jumamosi lilimsaka Wakili Kibatala
kwa njia ya simu ili kumsikia alichonacho
kufuatia kesi ya mteja wake kuanza
kusikilizwa ambapo alisema:
“ Tutakutana mahakamani jamani , kwa sasa
niko bize sana. ”
LULU
Juzi, simu ya Lulu ilipigwa kwa muda mrefu
lakini haikupokelewa huku baadhi ya watu
wake wa karibu wakisema kuwa, staa huyo
ameasisi tabia mpya ya kutopokea simu
zenye namba ngeni machoni mwake .

No comments:

Post a Comment