Saturday, February 08, 2014

Kanusho la Mh Lowassa kuhisiana na umiliki wa kurasa za mitandao ya kijamii

Kumekuwa na kurasa (accounts)
mbalimbali zenye jina la Mh. Edward
Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika
mitandao ya kijamii Kama vile
Facebook,Twitter,Instagram nk.
Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh.
Edward Lowassa.
Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote
hazimilikiwi na Mh. Lowassa.
Kwa maana hiyo chochote
kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye
kurasa hizo,hazihusiani kwa namna
yoyote na Mh. Lowassa.
Hata hivyo Mh. Lowassa anawashukuru
wote wenye kumiliki account hizo bila ya
ruhusa yake, kwani anaamini
wamesukumwa na mapenzi yao kwake.
Imetolewa na
Ofisi ya Mh. Edward Ngoyai Lowassa
Mbunge wa Jimbo la Monduli.

No comments:

Post a Comment