Monday, February 17, 2014

LULU AMEKIRI,ALIKUA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA KUNUMBA,HUU NDIO USHAIDI ALIOTOA MAHAKAMANI

MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth
Michael'Lulu' ambaye anakabiliwa na kesi ya
kumuua bila kukusudia msanii mwenzake,
Steven Kanumba, amekiri kuwa alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na
kwamba walikuwa na ugomvi.
Lulu alikiri hayo leo wakati akisomewa
mashitaka yake mbele ya Jaji Rose Temba wa
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es salaam
ambapo lulu baada ya kusomewa mashitaka
amekana kumuua.
Mbali na kukiri kuwa na uhusiano, pia lulu
akikiri kuwa baada ya tukio alitoka nje ya
chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia
mdogo wake Marehemu Kanumba, Setti Bosco
kuwa marehemu amedondoka.
Akisoma hati ya mashitaka Wakili Mwandamizi
wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7,
mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es
salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia
msanii Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo
mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa,
mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa
Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha
kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe
ndani ya ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano
pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi
unatarajia kuwa na mashahidi watano na
vielelezo.
CREDIT : PRO24

No comments:

Post a Comment