Mcheza filamu mwenye jina kubwa bongo Wastara Juma amesema kwa mwaka huu yuko bize na kazi kwa ajili ya kuwapa vitu vizuri mashabiki.wake na pia kwa ajili ya maisha yake na familia kwa ujumla
Wastara amesema hayo wakati akimfungukia muandishi wa habari hii nakuongeza kuwa kwa sasa hana muda wakufatilia furani kafanya nini bali anamuda wa kuwaza yeye atafanya nini ili asonge mbele
“Unajua kuna watu wako bize na maisha ya watu wakati maisha hayo yameshapita kila mtu anaangalia maisha yake binafsi sina muda na mambo ya mtu nafanya yangu“
Kwa kudhihilisha kuwa huu ni mwaka wake staa huyo anaesumbua bongo movie ameshafanya filamu mbili tangu mwaka umeanza uku rundo ya filamu alizoshiriki kutoka hivi karibuni
Wastara anatikisa soko la filamu kwa filamu yake ya Shaymaa na hivi karibuni anakuja na “Last Decision“(maamuzi ya mwisho)
No comments:
Post a Comment