Monday, January 27, 2014

PENNY:DIAMOND KAMA CHIZICHIZI VILE

MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten,
Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa
sifa ya aliyekuwa mpenzi wake , Nasibu
Abdul ‘ Diamond ’ ni kama chizichizi lakini
kwa undani zaidi ni mtu makini .

Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa
sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni
ambapo mbali na kutamka kauli hiyo ,
alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi
lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha
kwa kupeana nafasi .
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea
naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja
na ushee hivi, Penny alisema watu wote
wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile
kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa
mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano ,
anakuwa makini sana.
“ Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa
ndani ni mtu makini sana . Anajua kulea,
anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa
anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake
anapokuwa nyumbani, anajali , ” alisema
Penny na kuongeza :
Penny.
“ Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika
maisha ya kawaida ni tofauti kabisa ,
mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani
na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake
na si nyumbani .”
Katika aya nyingine , Penny alitiririka na
mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao
limetawaliwa na misukosuko , walikaa chini
kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya
kila mmoja wao kufanya mambo yake ,
hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake
kuwa sikutaki .
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu
vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za
Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya
kwanza nchini China , hakuamini hadi
walipokuja kukaa naye na kuzungumza
ndipo walipoamua kupeana nafasi .
Diamond .
Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa
Diamond amerudiana na Wema lakini yeye
kwa sasa ‘ bado yupoyupo sana ’, akakiri
kuwa anatongozwa na watu tofauti na
endapo ikitokea akaamua kuanzisha
uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu
kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri,
tofauti na zamani

GP

No comments:

Post a Comment