Mayasa Mariwata na Shani Ramadhan
MSANII mkongwe wa muziki wa dansi
Bongo, Muhidini Gurumo ambaye kwa sasa
amestaafu, amefungukia skendo ya kuwa na
mademu wengi inayomuandama Nasibu
Abdul ‘ Diamond ’ .
Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ .
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni maeneo
ya Ilala jijini Dar, Mzee Gurumo alisema :
“ Diamond ana nidhamu sana ila vile
anavyotamba jukwaani na kudatisha
mashabiki hapo ndipo balaa linapokuja,
watoto wa kike wenyewe wanaanza
kujisogeza kwake .
Mzee Muhidini Gurumo .
“ Pamoja na skendo za mademu
zinazomuandama , siwezi kumshusha
thamani, ana haki ya kujiopolea mwanamke
yeyote anayempenda, yeye kama
mwanaume rijali wakati mwingine ni vigumu
kujizuia na vishawishi hivyo.”
GP
No comments:
Post a Comment