Saturday, February 01, 2014

MAMA JOHARI AMFUMUA RAY

Makubwa! Kwa mara kwanza mama mzazi
wa mwigizaji mkongwe Bongo , Blandina
Chagula ‘ Johari’ ambaye hakupenda jina
lichorwe gazetini ameibuka na kumfumua
staa wa filamu ‘ mbia ’ wa mwanaye , Vincent
Kigosi ‘ Ray ’ ,
Mwigizaji mkongwe Bongo , Blandina
Chagula ‘ Johari’ .
Akizungumza na mapaparazi wetu katika
mahojiano maalum nyumbani kwake, Ubungo
External, Dar , wiki hii , mama Johari
alifunguka kuwa hamjui wala hajawahi
kumuona Ray ambaye ni mkurugenzi mwenza
wa Johari. Ndiyo wamiliki wa kampuni ya
kufyatua filamu ya RJ Productions.
Mama Johari ambaye pia ana makazi yake
mkoani Shinyanga alisema alitua jijini Dar
kwa matibabu ya presha .

Baada ya kumjulia hali, mapaparazi wetu
walitaka kujua mama huyo anamzungumziaje
Ray ambaye amekuwa akifanya kazi kwa
karibu na bintiye na kwamba ilishasemekana
ni wapenzi .
Ndipo mama huyo alipokuja juu akisema huyo
Ray mwenyewe hamjui na hajawahi kumtia
machoni zaidi ya kumsikisikia tu kama
wengine.
“Mimi simjui huyo Ray na wala sijawahi
kutambulishwa wala kuonana naye , kwanza
siishi hapa nitamuonea wapi , nimekuja zangu
kutibiwa tu kutokana na matatizo yangu ya
presha na kisukari .”
“Kwanza mwanangu hana muda wa kukaa
na kumuumizia kichwa huyo Ray kwani yeye
ni baba yake ?
“Hata siku moja ( Johari) hawezi kuishi kwa
kumtegemea yeye ( Ray ) , ” aliongeza mama
huyo.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa
sauti cha Risasi Jumamosi , mama huyo
alisema kamwe hawezi kuumiza kichwa
kuingilia mambo ya mwanaye , kwa kuhofia
maradhi aliyonayo na kujitia matatizoni kwa
mambo asiyoyajua undani wake.
Alisema anamshukuru Mungu kutokana na
hali ya mwanaye aliyekuwa anaumwa kupata
ahueni na kundelea na kazi zake .
Alipotafutwa Ray ili kuelezwa kile
alichokisema mama Johari, simu yake ya
kiganjani iliita bila kupokelewa

GP

No comments:

Post a Comment