THE Ijumaa Sexiest Girl 2012 , Jacqueline
Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa
na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha
kwa jina la G Modo akiamini atampoza
machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi
wake wa zamani , Abdallah Mtoro ‘ Dallas’
huku akiwatahadharisha mashosti zake
kutoleta shobo (kuwa mbali naye ).
Jacqueline Wolper .
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni,
Wolper alisema anafikia hatua ya kusema
hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye
amegundua ni mwanaume anayejitambua
na anayeheshimu mapenzi ila akawataka
mashosti zake kutomsogelea .
“ Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni
mwenye furaha kubwa , nasahau hata yale
machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa
zamani . Lakini najua wapo wanaomtolea
macho , tusitafutane ubaya, kila mtu na
maisha yake , ” alisema Wolper.
GP
No comments:
Post a Comment