Monday, January 13, 2014

Kuzaa sio rahisi:Rose Ndauka

WIKI tatu tangu ajifungue mtoto wa kike, staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema amejifunza tendo hilo siyo la mchezo na kugundua kuwa mama anapaswa kuheshimiwa.

Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Rose alisema kutokana na jinsi anavyohitajika kumhudumia mtoto, watu wote wanapaswa kumheshimu sana mama kwani kuzaa na kulea siyo mchezo.

“Mtu asikuambie kitu jamani, mama ni kitu kingine, nilivyozaa ndiyo nimeona mama ni kila kitu maana sasa hivi usiku silali kutokana na kumuangalia mwanangu,” alisema Rose aliyempa mwanaye jina la Naila.

GP

No comments:

Post a Comment