Monday, January 13, 2014

Pub ya Aunt Ezekiel chali

PUB iliyoibuka kwa muda mchache na kukamata ‘taito’ kubwa Bongo ya mwigizaji Aunt Ezekiel, Demonte imefungwa ghafla, haitoi huduma

Imedaiwa kuwa, pub hiyo iliyopo maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar, imefungwa kutokana na mhusika kushindwa kuiendesha.

“Imefungwa, nasikia gharama za vinywaji na wafanyakazi aliowaajiri zilikuwa juu akaona bora afunge,” alisema rafiki wa Aunt aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Paparazi wetu alishuhudia pub hiyo ikiwa imefungwa kwa zaidi ya miezi kadhaa, alipomtafuta Aunt, hakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

GP

No comments:

Post a Comment