Tuesday, December 31, 2013

Simshangai Wema kurudiana na Diamond:Yuster Nyakachara

Muigizaji na mmiliki wa kampuni ya Eagle Intertaiment inayojishugulisha na utengenezaji wa filamu Yuster Nyakachara amesema hajamshangaa Wema Sepetu kurudiana na mwanamuziki Diamond kwakua penzi la kweli halifi

Akiongea na blog hii mrembo huyo anaekuja juu kwa kasi amesema inaonekana Wema anapenzi la dhati kwa Diamond ndio maana amesahau vituko vyote alivyofanyiwa ikiwa ni pamoja na kudaiwa kurekodiwa sauti akimbembeleza Wema na kukataa pesa alizotunzwa kwenye show ya Mlimani city

Ata hivyo amesema mambo hayo ni yakaeida ata mtaani kuna watu wengi wanafanyiana matukio ya ajabu kushinda hayo lakini mwisho wa siku wanarudiana

Yuster hivi karibuni atakuja na filamu yake ambayo inaitwa Majuto si hasara akiwa na Jackline wolper pamoja na Slim na wengine wengi

No comments:

Post a Comment