Baada ya msaani wa filamu nchin Salma Nisha kuipata akaunti yake ya mtandao wa kijamii facebook uliokua umeibiwa na wezi wa mtandao iki ndio amekiandika
Miaka mitatu ya kuhangaika kupata mafanikio.. mwaka mmoja baada ya kuweza kuonesha kile nilichonacho na kukihangaikia,M'Mungu akanipa mashabiki waliokubali kile ninachofanya.. siku zote huwa naamini kazi zangu ndizo zitanitengenezea mashabiki,heshima na jina,huwa naamini scandal siku zote humshushia hadhi mtu,iwe msanii,au mtu wa kawaida.. niliyopitia ni mengi ila baada ya kujitambua nikakaa nilipo na hapo ndipo nikawaona wanaonipenda wakinifata na kussuport.. mfano NESI SELENA,TIKISA,PUSI NA PAKU ,MATILDA na nyngn nyingn naona matunda yake,but mtu anaamua kukaa siku moja tu kuamua kumchafulia mtu jina alilolitengeneza na kuligharamikia kwa miaka kadhaa,kiukweli ktk siku niliyoumia leo nimeumia sana,ila siachi kumshukuru Mungu wangu sababu ananionesha jinsi ya kuishi na walimwengu wakoje,ahsante Mungu.. nimeirudisha account chini ya mikono yangu.narudia tena SAMAHANINI SANA KWA PICHA ZILIZOHARIBU UTU WETU.naomba munisamehe mimi maana ndio page yangu na nyinyi hamkujua.. na mm naamini kuwa siku zote mja mwema ni mwepesi wa kuomba radhi hata km hajakosea yeye ili nafsi za watu zisiwe na kinyongo.. NAOMBA MUNISAMEHE ALIYEPOST PICHA SIO MIMI.. na picha ya mwanamke nusu uchi waliyomficha uso pia SIO MIMI. . kwanza yule mweusi mimi mweupe.
No comments:
Post a Comment