NDO basi tena! Staa wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho
‘Maya’ amefunguka kuwa kwa sasa amejikita katika kupiga kazi za nje ya
Kampuni ya Kanumba The Great Film hivyo asiulizwe kuhusu kampuni hiyo
aliyofanya nayo kazi kwa muda mrefu.
Maya alitiririka kuwa ameamua kuiweka kando kampuni hiyo na kujikita katika kazi za nje na ikiwezekana asimame mwenyewe.
“Nipo nje ya kampuni kwa sasa, kampuni inaongozwa na mama Kanumba
(Flora Mtegoa) mwenyewe, nafanya kazi na watu tofautitofauti ili baadaye
nisimame mwenyewe,” alisema Maya.
No comments:
Post a Comment