Baada ya maswali ya muda mrefu na kwamba ndoa hakuna, hatimaye
mipango kabambe ya ndoa ya staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus
Ndauka na mchumba’ke, Malick Bandawe imekamilika ambapo sasa siku
zinahesabika.
Kwa mujibu wa Malick ambaye pia ni msanii, kulikuwa na maandalizi
ambayo yalikuwa yakiendelea hivyo kwa sasa kila kitu kipo sawa na
kinachosubiriwa ni kugawa kadi ambazo zitakuwa zinaonesha tarehe ya
ndoa.
“Sasa hivi dogo amekua, anaweza kufanya fujo mbili-tatu hivyo
kinachofuata ni ndoa, kadi zitaanza kugawanywa soon,” alisema Malick
ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na Rose Ndauka.
No comments:
Post a Comment