Wednesday, July 02, 2014

Edward Freedom:moja ya ndoto zangu ilikuwa kucheza filamu na Wastara na nimetimiza

Mcheza filamu anaeaminika atakuja kuteka soko la filamu nchini kutokana na umahili wake wakuigiza Edward Freedom amesema moja ya ndoto zake nikucheza filamu na Wastara Juma jambo ambalo amelitimiza

Kijana huyu kutoka Mwanza ambaye amecheza filamu kadhaa na mastaa kibao bongo amesema alijisikia faraja sana alipokuwa anacheza filamu na mrembo huyo ambae anasumbua sana nchini kutokana na uwezo wake wakuigiza filamu za majonzi

"kwenye filamu ya Last Decisioni nimecheza vizuri tena kwa kiwango kikubwa sana  nimoja ya filamu ambazo ikitoka itakuwa gumzo sana mtaani"

Hiyo ni kauri yake Edward baada ya kuulizwa kuhusu filamu aliyocheza na Wastara,na ikumbukwe filamu hiyo inatarajia kutoka hivi karibuni ikiwa na mastaa wengi wenye uwezo akiwemo Hemed Suleiman

No comments:

Post a Comment