MASTAA wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Sabrina
Rupia ‘Cathy’, Salma Salim ‘Sandra’ na Rose Ndauka juzi walikuwa kivutio
kwa wananchi waishio maeneo ya Kinondoni jijini Dar baada ya kushindana
kuzungusha nyonga.
Staa wa filamu Bongo Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Mastaa hao walifanya tukio hilo katika sherehe za kuwasimika ukamanda wa
vijana Tawi la CCM Bwawani ililopo maeneo hayo wakati walipopagawa na
vikorombwezo vya Msaga Sumu katika wimbo wa taarab.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Dah kumbe mastaa wetu wana fani nyingi, angalia mauno yale utafikiri
hawana mifupa sehemu za kiunoni,” alisikika akisema njemba moja
lililokuwa likishuhudia shoo hiyo ya bure.
Staa wa filamu Bongo, Salma Salim ‘Sandra’.
chanzo globalpublishers
No comments:
Post a Comment