Habari mpya kama sio njema ni kuwa Wema Sepetu na Kajala Masanja
wamemaliza tofauti zao zilizotokana na ‘beef’ lao lilichukua week kibao
sasa. Kwa mujibu wa taarifa mpya mitandaoni ni kuwa mastaa hao wawili
ambao waliwahi kuwa mashosti wakubwa walimaliza ‘beef’ lao katika
sherehe ya kibao kata cha mwandishi wa magazeti ya Globalpublishers
anayeitwa Imelda Mtema.
Katika tukio hilo mastaa kibao walihudhuria akiwemo Aunty
Ezekiel ambaye kwasasa amekuwa karibu zaidi na Wema Sepetu. Nae Wema
Sepetu kupitia Instagram ame-share picha hiyo hapo juu akiwa na kina
Kajala na kuandika "nawapenda sana hawa hapa..jana hiyo kwa kibaokata
cha Imelda Mtema"
No comments:
Post a Comment