Tuesday, April 08, 2014

KAJALA AFUNGUKA KWA UCHUNGU KUHUSU BEEF LAKE NA WEMA NA KUTUKANWA NA TEAM WEMA

Kajala Masanja ambaye ni star wa filamu
Swahiliwood amefunguka kuwa hana tatizo na
Wema ila anashangzwa sana kutukanwa matusi
ya nguoni na "Team Wema" katika mitandao ya
kijamii hasa Instagram kiasi cha mwanae
aitwaye Paula kuona matusi hayo na kujisikia
fedheha. Inadaiwa kuwa Kajala na Wema
kwasasa hawapo katika urafiki mzuri kama
zamani na zile millioni 13 alizowahi kulipiwa
kama faini na Wema ili asifungwe gerezani
zimekuwa kama wimbo wa taifa kwa team
Wema kwenda kwa Kajala wakimtaka
azirudishe.

Vile vile inadaiwa kuwa wiki ilopita Wema na
Kajala walikutana katika ukumbi wa Maisha
Club uliopo Masaki na kushindana kumtunza
Snura aliyekuwa na show lakini team Wema
walipomuona Kajala wakaanza kutaka
kuanzisha vurugu huku team Kajala nao
wakijibu mapigo na kumlinda Kajala aliyetaka
kuondoka eneo hilo kuepusha shari.
Kajala alipoulizwa na Globalpublishers kuhusu
tukio hilo alikana kulishuhudia ila alikiri
kutokuwa katika uhusiano mzuri na Wema kwa
kusema "Mimi kwa upande wangu sina tatizo
na Wema lakini natukanwa sana bila sababu.
Sijui nimemfanyia nini kibaya, narudia tena
sina tatizo na Wema halafu siyo yeye
anayenitukana au kunisakama, ni kundi
linalojiita TeamWema, sina uhakika kama yeye
ndiye anawatuma, kuhusu milioni 13, sasa
nitazirudishaje wakati hakunikopesha, alinilipia
bure? Hata sijui kama nikizirudisha nitakuwa
sahihi? Sielewi lakini kama ni matusi, kweli
natukanwa sana hadi mwanangu anaona
ninavyoitwa malaya" alikaririwa Kajala akisema
kwa uchungu mkubwa.

No comments:

Post a Comment