Wednesday, March 12, 2014

WEMA SEPETU ALIA KUPATA MTOTO

MASKINI ! Kilio kikubwa cha Wema Isaac
Sepetu ni kupata mtoto , Risasi
Mchanganyiko linafunguka.
Habari zilieleza kuwa Wema amekuwa na
kiu ya mtoto kwa muda mrefu na kwamba
alishakuwa na wanaume tofauti lakini
hawakumpatia mtoto.
Ilisemekana kwamba katika msururu wa
wanaume aliominya nao kimalavu , iliwahi
kuripotiwa kuwa ni mwanaume mmoja tu
aliyefanikiwa kumpa ujauzito lakini kwa
bahati mbaya mimba ilichoropoka .
Mwanaume aliyekuwa na mzigo huo ilidaiwa
ni Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica ,
Charles Gabriel ‘ Chaz Baba ’ .
Baada ya kupania kwa muda mrefu bila
mafanikio , ilidaiwa kuwa mwanadada huyo
mkali wa sinema za Kibongo aligeuzia
mapenzi yake kwa mbwa (pets ) wake wawili,
Van na Gucc ambao mmoja wao amezaa
hivi karibuni.
Habari zinadai kuwa, kutokana na mapenzi
yake na mbwa hao , amekuwa
akiwagharamia mkwanja mrefu katika
chakula na shopping za mavazi ya bei
mbaya.
WEMA ANAFAFANUA
“ Nawapenda sana mbwa wangu , nawaona
kama ndiyo watoto wangu kwani sina mtoto
na ninatamani sana ila najua Mungu
atanijalia siku moja muda ukifika , ” alisema
Wema na kuongeza:
“ Kila jambo na wakati wake , nitapata tu,
nadhani ni suala la muda tu. Watu
wanaweza kushangaa namna
ninavyowapenda mbwa wangu,
nawathamini kwa sababu wananipa faraja
na nipo nao karibu . Nawajali kama
binadamu .”
Kabla ya Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz ’
anayetoka naye kwa sasa, wengine
waliowahi kuonja penzi lake na
wakashindwa kumpatia mtoto ni pamoja na
marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf
na Chaz Baba

No comments:

Post a Comment