Friday, March 14, 2014

Huyu ndio Wastara Juma Issa

Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996 alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo,

Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na filamu yake yakwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini King Majuto
Wastara akiwa na King Majuto                                                                                                 







Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV AKUTANA NA JENIFA MGENDI
Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.
Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara.
AKUTANA NA SAJUKI
Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.
Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta (Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.
 “Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.
FILAMU WALIZOZALISHA
Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu mkubwa
 APATA AJALI
Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.
Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.
Juni mwaka huohuo,
wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.
Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo

tarehe 2 mwezi wakwanza mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa 
Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania

1 comment:

  1. Pole sana Wastara hizo ni changamoto za maisha na tumeimbiwa binaadamu.Hongera wewe ni msanii mzuri sana,napenda sana kazi zako.

    ReplyDelete