IMEBAINIKA kuwa ndani ya tasnia ya
filamu Bongo kuna baadhi ya wasanii
wanaofanya mapenzi ya jinsia moja yaani
mashoga , Risasi Mchanganyiko
limenyetishwa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven
Mengere ‘ Steve Nyerere’ .
Hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya
Rais wa Uganda, Yoweri Museven , kupitisha
sheria nchini mwake ya kupiga marufuku
mavazi yasiyo na staha , uvunjifu wa maadili
na mapenzi ya jinsia moja .
Uganda ipo katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki ikiunganishwa na nchi za
Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na
Uganda yenyewe.
Dk . Cheni .
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo
ndani ya kundi hilo , baadhi ya wasanii wa
kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga , ingawa
wanajifanya vidume vya mbegu .
“ Wapo mashoga na mabwana zao
tunawajua ila sema sasa kwa sababu huna
ushahidi wa moja kwa moja na hujamfuma
kwenye tukio , unashindwa kumtaja , ”
alisema msanii mmoja wa kike, Bongo.
“ Yule …(analitaja jina la msanii mkubwa )
bwana ’ ke alifariki na sasa ana mwingine
lakini ndani ya Bongo Muvi anaonekana
kiwembe kwa sababu ana msururu wa
wanawake, ” alisema .
Msanii Hisani Muya ‘ Tino ’ .
AMSHAURI JK
“ Ingekuwa vyema sana kama Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akafanya kama alivyofanya
mwenzake wa Uganda , Yoweri Museven
katika kupiga vita ushoga, ” alipendekeza
msanii huyo .
Msanii mwingine wa kike ambaye amekuwa
kwenye tasnia hiyo tangu enzi za makundi
ya sanaa kutamba runingani (jina kapuni)
naye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo lakini
akadai wanafanya kwa siri sana.
“ Kuna wasanii wanaonekana watanashati
mbele ya jamii lakini ni chakula ya watu
kwa kuwa wanapenda sana vitu vya bure , ”
alisema msanii huyo na kuongeza:
“ Wapo wengi tu ndiyo maana katika maisha
yangu sijawahi kutoka na mwanaume wa
Bongo Muvi , ni wachafu sana . Siku zote
wasanii wa kike ndiyo tunaoambiwa kuwa ni
malaya , eti tuna tamaa na habari nyingi
zinatuchafua siye lakini ukweli ni kwamba
hata wanaume wana tamaa ya maisha
mazuri na mwishowe wanageuzwa
wanawake.”
Ray Kigosi .
HUYU YUPO TOFAUTI NA WENZAKE
“ Sikia nikuambie, ni kweli hili suala lipo
lakini si kwa wote na kuna baadhi huwa
wanasingiziwa tu. Unajua nini ? Unaweza
kukuta mtu ana tabia tu ya kujipenda , lakini
wengine wanasingizia kuwa eti ni mashoga –
siyo kweli .
“ Mfano hata uje na greda hapa, akitokea
mtu anazungumza upuuzi eti JB , Dk . Cheni ,
Ray, Hemed PHD, Mlela au Dude ni
mashoga , nitabishana nao mpaka mwisho.
Hao ni watu ambao wanajipenda tu, sasa
ukiwahusisha na huo ujinga nitashangaa
sana. Sisemi kuwa wanatajwa ila sasa
akitokea mjinga akaja na hoja hiyo,
nitabishana naye , ” alisema msanii mmoja
ndani ya Bongo Muvi .
Msanii JB .
Msanii Hisani Muya ‘ Tino’ aliwahi kuigiza
kama shoga na kusababisha minong ’ ono
kwenye jamii , katika filamu aliyoipa jina la
Shoga lakini ilizuiwa na serikali.
Mwingine ni Dk . Cheni ambaye amecheza
kama shoga kwenye filamu yake ya
Nimekubali Kuolewa , ingawa bado haijatoka
mpaka sasa.
Msanii huyo akizungumzia hayo , alisema:
“ Kucheza filamu kama shoga hakuna maana
kuwa kweli ni shoga , ni kuvaa uhusika tu.
Watu wasiwahusishe wasanii walioigiza
kama mashoga kwenye hii skendo , ” aliweka
nukta msanii huyo mwenye maneno mengi.
WASIKIE WENYEWE
Baada ya kupata taarifa hizo , waandishi
wetu waliwatafuta baadhi ya wasanii wa
kiume Bongo wanaotesa na kuwauliza
kuhusu ishu hiyo (wasanii hao hawamo
kwenye orodha tuliyonayo ).
Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Mahsein
Awadh ‘ Dk . Cheni ambaye alisema : “ Miye
sina la kusema kuhusu hilo, ni vyema kama
utamtafuta mwenyekiti ( Bongo Movie Unity,
Steve Nyerere) ndiye mwenye mamlaka ya
kuzungumza masuala kama hayo. ”
Msanii Kulwa Kikumba .
KULWA KIKUMBA ‘ DUDE ’
“ Hilo suala la ushoga ndani ya Bongo Muvi
lipo hata miye nalisikiasikia, lakini halina
uthibitisho ila kusemwa linasemwa sana. ”
STEVE NYERERE
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven
Mengere ‘ Steve Nyerere’ : “ Ni kweli taarifa
hizo zipo , wasanii wakishakunywa pombe
huwa wanafanya mambo ya ajabu sana
kuashiria tabia zao halisi , mimi kama
mwenyekiti wa Bongo Movie huwa ninaumia
sana.
“ Nitahakikisha nawafukuza mashoga wote
hata kama tutabaki wawili katika kundi letu,
bora wawe na heshima. ”
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
MWAKIFWAMBA SASA
Tanzania ‘TAFF ’,
Simon Mwakifwamba : “ Hiyo ishu ni kweli
ipo, ndani ya Bongo Muvi, mashoga wapo
wengi sana , ila bado hatujapata ushahidi wa
kuweza kuwataka hadharani .”
No comments:
Post a Comment