Thursday, February 13, 2014

WEMA:PIGA,UA LAZIMA DIAMOND ANIOE

Licha ya mama yake mzazi kupinga kwa
nguvu zote, staa wa filamu nchini na
mtangazaji wa Kipindi cha Runinga cha In
My Shoes , Wema Sepetu ameapa kwamba
hata iweje , lazima msanii maarufu wa
muziki wa kizazi kipya nchini , Nasibu Abdul
‘Diamond ’ awe mume wake , Amani lina stori
kamili.
Wema akiwa na mpenzi wake Diamond .
NI CHAGUO LAKE
Akizungumza na Amani katika spesho
intavyu hivi karibuni, Wema ambaye kwa
sasa anapika na kupakua na Diamond
alifunguka kuwa, amepita kwa wanaume
wengi ila anaamini mwanaume huyo ndiye
chaguo lake .
Alisema katika uchunguzi wake aligundua
kwamba Diamond anampenda kupita
maelezo na kwa mapenzi anayomuonesha
hana sababu ya kugoma kumpa nafasi ya
kuwa mkewe .
Wema na Diamond katika pozi la
kimahaba .
“ Yaani watu watasema sana lakini piga, ua ,
garagaza, lazima Diamond anioe . Amekuwa
akilizungumzia hilo na kuonesha kuwa yuko
‘siriasi ’ hivyo ipo siku historia itaandikwa bila
kujali nani atasema nini .
“ Unajua mimi ni mtu ninayejitambua na
ninayejali maisha yangu hivyo ninapobaini
mwanaume f ’ lani anaonesha kunijali na
kunipa mapenzi ninayoyahitaji , kwa nini
nisikubali kuingia naye kwenye maisha ya
ndoa…?
“ Kwa kifupi nampenda Diamond na yeye
ananipenda , that ’ s it , ” alisema Wema .
MKWARA WA MAMA YAKE
Kuhusu mama yake kuchimba ‘biti ’ kuwa
hamtaki Diamond na kamwe hawezi
kukubali mwanaye aolewe na mwanaume
huyo , Wema alisema:
“ Unajua yule ni mzazi , wakati mwingine si
mbaya kuonesha hisia zake lakini nitamseti
na naamini kwa kuwa ananipenda
atakubaliana na mawazo yangu . ”
NDOA LINI ?
Alipobanwa kuhusu lini watafunga ndoa
kwani wamekaa kwenye uhusiano kwa
muda mrefu huku wakiachana na
kurudiana , Wema alionekana kutokuwa na
jibu la moja kwa moja ila akaishia kusema
kuwa, siku ikifika kila kitu kitakuwa wazi.
NUKUU YA MAMA WEMA !
Katika sakata hilo, kwa upande wake mama
Wema alikuwa na haya ya kusema : “ Ndoa
yao watafungia chumbani, si hadharani,
tena wakiwa na ndugu wa upande mmoja
tu wa Diamond .
“ Sisi hatuwezi kushiriki ng ’oo , ndugu zangu
wakijitokeza tu nitakuwa na panga
mkononi , watakiona cha moto .”
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011 ndani ya Ukumbi wa New
Maisha uliopo Masaki , Dar, Diamond aliwahi
kumvisha pete ya uchumba Wema na
ikadaiwa kuwa siku nyingi wangeingia katika
maisha ya ndoa lakini haukupita muda
mrefu wakaachana .
Baada ya kumwagana , Diamond alikwenda
kwa mtangazaji wa DTV , Peniel Mungilwa
‘Penny’ na Wema alihamishia penzi kwa yule
kigogo aliyefahamika kwa jina moja la
Clement ‘ CK’ kabla ya kumwagana hivi
karibuni

No comments:

Post a Comment